Tuesday, January 31, 2012

Twiga Starz yaikandamiza timu ya TaIifa YA Namibia 5-2

Wachezaji wa timu ya wanawake Twiga starz wakishangilia

Mwanahamisi Omari Gaucho akiruka daruga la wachezaji wa Namibia

Kikosi cha Twiga starz

Asha Rashidi Mwalala akipiga shuti kuelekea golini mwa Namibia


Posted by Hija Mkali

Friday, January 27, 2012

Mh. John Mnyika aungana na madaktari

Na Frank Kimaro
                                            Waraka wa mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Myika

 Mgomo wa madaktari unaoendelea hivi sasa umedhihirisha kwamba tuna serikali dhaifu yenye ombwe la uongozi. Haiwezekani wananchi wakawa wanakufa kwa kukosa matibabu stahiki na wengine wakipata madhara kutokana na kuchelewa kupata matibabu sababu ya mgomo wa madaktari halafu viongozi wenye dhamana hawachukui hatua sahihi.
Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye mwenye dhamana kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 33 ndiye kiongozi wa shughuli za serikali na ibara ya 35 shughuli zote za utendaji wa serikali zinatekelezwa na watumishi wa serikali kwa niaba ya Rais; ameondoka kwenda nje ya nchi mgomo ulipoanza na hakuna kauli yoyote mpaka sasa toka kwa Makamu wa Rais wala kwa Ikulu.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda badala ya kwenda kwenye eneo la mgomo na kuzungumza na madaktari naye ameishia kuzungumza na vyombo vya habari. Waziri wa Afya Dk. Haji Mponda na Naibu Waziri Dk. Lucy Nkya nao jana wamezungumza na waandishi wa habari badala ya kwenda kukutana na madaktari na kuzungumza nao kuhusu madai yao ya msingi.

Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika

Kwa upande wetu CHADEMA tulitoa kauli tarehe 25 Januari 2012 ya kutaka serikali ichukue hatua na tuliona tuipe serikali nafasi ifanye kazi yake hata hivyo serikali haionyeshi kuupa uzito unaostahili mgogoro huu wenye kuathiri hali za wagonjwa na maisha ya wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Tuliacha kwenda katika eneo la mgomo kukutana na madaktari katika siku za awali kuepusha suala hili kutafsiriwa kuwa ni la kisiasa. Hata hivyo, kuchelewa kwa serikali kukutana na madaktari kunahitaji hatua za pamoja. Dhamira yangu kama mwananchi, mbunge katika mkoa wa Dar es Salaam na kiongozi wa chama cha siasa naumizwa na hali inayoendelea. Ni vigumu kuweza kuendelea na majukumu ya kibunge na ya kichama katika masuala mengine wakati serikali iko legelege katika suala ambalo linahusu uhai wa wananchi wenzangu uko mashakani.

Hivyo nawajibika siku ya leo kuelekeza nguvu katika kuungana mkono na madaktari katika madai yao ili kuishinikiza serikali kuweza kutuma ujumbe mkubwa kukutana na madaktari leo au kesho. Na iwapo serikali haitakutana nao katika muda huo, itabidi uongozi wa kambi ya upinzani bungeni ukiwa ni serikali kivuli na uongozi mkuu wa CHADEMA ukiwa ni chama mbadala kuweza kukutana nao.

Natambua kwamba uzembe na ufisadi katika serikali kwenye sekta ya afya unaligharimu taifa na maisha ya wananchi. Hivyo, CHADEMA inaitaka serikali kukamilisha kwa haraka majadiliano na madaktari na kutimiza madai yao ili kuepusha madhara zaidi kwa umma.

Nawapa pole wananchi ambao wameathirika na migomo inayoendelea na kuzingatia kwamba mgomo huo umesababishwa na udhaifu katika serikali.

Natoa mwito kwa umma wa watanzania kuwaunga mkono madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya katika hospitali na zahanati za umma kama sehemu ya kuboresha huduma katika maeneo husika.

Madai ya madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya nchini yasiposhughulikiwa kwa wakati na kwa ukamilifu watumishi husika wanaweza wasiwe kwenye mgomo wa wazi kama ilivyo kwa baadhi ya hospitali na zahanati nchini lakini wataendelea na migomo baridi kwa kutoa huduma mbovu au kuacha kazi kwenye maeneo ya umma na wengine kwenda kufanya kazi nje ya nchi wakati kukiwa na uhaba wa watumishi nchini.

Aidha, pamoja na migomo inayoendelea, naendelea kutoa rai kwa madaktari na watumishi wengine wa umma kuhakikisha maisha ya wagonjwa walio katika hali ya hatari yanaokolewa.

Nimezungumza na viongozi wetu wakuu kuhusu suala hili na natoa mwito kwa wadau wote kuunganisha nguvu katika kuisimamia serikali kushughulikia madai ya madaktari na wafanyakazi wengine wa sekta ya afya kwa haraka ili kuepusha madhara zaidi kwa umma.

Wananchi wenzangu wa Jimbo la Ubungo na umma kwa ujumla uzingatie kwamba tangu Mwalimu Nyerere aondoke madarakani mwaka 1985, Serikali ya CCM imeongeza wingi wa majengo mbalimbali kwenye sekta ya afya hata hivyo imeshindwa kusimamia utoaji bora wa huduma za afya katika zahanati, hospitali na vituo vya afya. Kutokana na mfumo mbaya wa usimamizi wa sekta ya afya, misingi imara ya kuimarisha sekta ya afya iliyowekwa baada ya uhuru imevunjwa na kubomolewa ikiwemo katika masuala yanayohusu kujali maslahi ya watumishi wa umma katika sekta hii muhimu.

Hali hii imefanya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa na nakisi ya watumishi asilimia 48% na takwimu zinaonesha kuwa 18% ya wafamasia, 15% ya madaktari, 13% ya madaktari wasaidizi waliacha vituo vyao vya kazi na kwenda kutafuta kazi kwenye mashirika ambayo yanalipa mishahara mikubwa na mizuri. Nakisi hii itaongezeka zaidi iwapo madai ya msingi ya madaktari na watumishi wengine hayatashughulikiwa na serikali itaendelea kuchelewa kushughulikia migogoro na migomo mingine inayoendelea.

Ni imani yangu kwamba serikali ikiwa na dhamira inaweza kuongeza mishahara kwa watumishi wa sekta ya afya ili kuweza kuwavutia wataalamu kubakia nchini badala ya kwenda kugoma au kwenda kutafuta kazi nje ya nchi kutokana na malipo mazuri huko. Hii ni pamoja kuwezesha malipo ya mazingira magumu kutolewa kwa watumishi wa afya wanaofanya kazi katika maeneo na kada maalum.

Kwa sababu hii, leo sitashiriki kikao cha Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kinachoendelea ili kupata wasaa wa kufuatilia kwa karibu suala hili na kuwasiliana na viongozi wenzangu kwa ajili ya hatua zaidi za pamoja.

Monday, January 23, 2012

WAZIRI MKUU MHESHIMIWA MIZENGO PINDA ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TENKILOJIA CHA NELSON MANDELA MKOANI ARUSHA

  
                               Waziri mkuu mheshiwa  Mizengo Pinda akiwa na baadhi ya viongozi wakikagua  maendeleo ya ujenzi  wa chuo kikuu cha Nelson Mandela leo.          
                                                                                                             Na Consolata    Haule

Sunday, January 22, 2012

DK SLAA ANA KWA ANA NA RAIS KIKWETE IKULU.


Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa, Ikulu Dar es Salaam jana usiku katika muendelezo wa mazungumzo ya mchakato wa Katiba mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe na katikati ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Said Alfi. Picha na IKULU


RAIS Jakaya Kikwete amekutana na uongozi wa Chadema Ikulu Jijini Dar es Salaam, akiwemo Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa, kuzungumzia mchakato wa Katiba Mpya.Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili, mkutano huo ulifanyika jana kuanzia saa 10:30 jioni na kuendelea hadi usiku, lakini walifanya mapumziko mafupi saa tatu usiku.


Ujumbe wa Chadema uliokuwa wa watu wanane, ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe. Wengine waliofuatana naye pamoja na Dk Slaa ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, John Mnyika, Said Arfi, John Mrema, Profesa Mwesiga Baregu na Profesa Abdallah Safari. Hadi tunakwenda mitamboni kikao hicho kilikuwa kinaendelea.


Hii ni mara ya kwanza kwa Dk Slaa kukutana na Rais Kikwete tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2010, ambao Dk Slaa alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34 akiwa nyuma ya Rais Kikwete aliyepata kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17, Dk Slaa hakuwahi kukutana na mkuu huyo wa nchi ana kwa ana.
               
POSTED BY SIXTUS BAHATI.



ELIMU INA MAMBO!


POSTED BY SIXTUS BAHATI.

Saturday, January 21, 2012

BAJ WATANDAZA KANDANDA SAFI DHIDI YA MAENDELEO YA JAMII

Na Solomon Lekui
Full beki ya timu ya BAJ1 OLE LEKUI

Katika kuonesha kwamba timu ya wanafunzi wa Bachelor of Arts in Journalism kimejizatiti vizuri katika mpira wa miguu ( football) jana timu ya mwaka wa kwanza ilionesha kandanda la kitabuni baada ya kucheza pasi nyingi na safi zilizoifanya timu ya wapinzani wao BACD kuomba mechi kumalizika kabla ya wakati baada ya kuchoshwa na kandanda safi liloneshwa na vijana wa BAJ1. Mchezo huo ulianza kurindima kwenye mishale ya saa 11 na kumalizika saa moja kasoro.

Pamoja na kuonesha kandanda safi timu hizo zilitoka suluhu ya kufungana magoli 2-2 lakini mchezaji mmoja wa BACD aliumia vibaya sehemu za mbavu tukio lililopelekea kulazwa katika hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi.
Mashabiki nao hawajaachwa nyuma kwa kushangilia na kutia moyo huku wakiimba nyimbo za uhamasishaji kama vile "usiniumizieeeee....." watu weweeeeee                                      



wachezaji wa BAJ oscar,zephania pamoja na goalkeeper on duty waisaka chacha a.k.a "MURA"
Hawa ndio baadhi ya wachezaji wa timu ya BAJ kutoka kulia ni Oscar a.k.a mzee wa kiatu, katikati ni hija mkali a.k.a panya buku na ole lekui a.ka. beki mstaarabu

Hii ni baada ya mechi wachezaji wakajiunga na mashabiki wao kucheza kiduku

MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA KIISLAMU CHINI YA ULINZI MKALI WA POLISI

Na Solomon Lekui


Waziri wa elimu Dk. SHUKURU KAWAMBWA akizungumza na wanafunzi wa kiislamu jijini Dar es salaam katika maeneo ya kidongo chekundu
Dk. SHUKURU akiondoka maeneo hayo chini ya ulinzi mkali wa polisi


wanafunzi na mabango mbali yenye jumbe mbalimbali






Wanafunzi wa kiislamu shule za sekondari za Dar es salaam wameandamana jana kama walivyoahidi siku chache zilizopita kwenye vyombo vya habari. Maandamano yao yaliishia viwanja vya kidongo chekundu na waziri wa elimu Dk.shukuru kawambwa alikuwepo kuongea nao.


Friday, January 20, 2012

HATUKO NAE TENA ALIYEKUWA NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MBUNGE WA ARUMERU MH; JEREMIAH SUMARI

   Ni masikito na huzuni kubwa kwa wananchi wa Tanzania kupoteza mmoja wa watu mashuhuri Tanzania ambaye alikuwa mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia chama tawala (CCM) na naibu waziri wa Fedha wa awamu ya nne kupitia uongozi wa Mh. Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE.              
                 Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa SARATANI YA UBONGO kwa muda mrefu  sana na mnamo mwaka 2010 aliweza kumpelekwa nchini INDIA kwa matibabu zaidi ya upasuajina aliweza kupata nafuu.Mwishoni wa mwaka 2011 hali yake ilianza kuwa tete tena na tarehe 9,January,2012 alilazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili  ambapo siku ya alhamisi ya tarehe 19,January,2012 alitutoka duniani.



                                                      MAREHEMU JEREMIAH SUMARI.



                   Hivyo kutokana na msiba huo kamati ya bunge kushirikiana na familia na chama chake (CCM) wameandaa shughuli nzima ya kuuaga rasmi mwili wa marehemu siku ya Jumamosi tarehe 21,January katika viwanja vya KARIMJEE kuanzia mida ya saa 5 asubuhi  na siku ya jumapili kuweza kusafirisha kuelekea kijijini kwao     AKERI,MERU,mkoani ARUSHA kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika siku ya Jumatatu ya tar 22,january.2012.

                     Marehemu ameacha mjane na watoto wanne(4).     
                    
                               MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU 
                                              MAHALI PEMA PEPONI.
                                                         AMINA.
       "BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA  LIBARIKIWE"
                                                                                                                       Na Consolata Haule

Thursday, January 19, 2012

MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI HATUNAE TENA

TAARIFA zilizotufikia katika muda huu zimethibitisha Mbunge wa Jimbo la Arumeru kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Jeremia Sumari, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hopitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa ugonjwa wa Kansa ya kichwa. Bwana alitoa na Bwana ametwaa Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, amina
                                                                                                                               Na Solomon Lekui

Tuesday, January 17, 2012

IN PICTURES TOKA KARIMJEE - Buriani Dada REGIA MTEMA

Na solomon Lekui

Ama kwa hakika dada yetu mpendwa ulipendwa na wengi kama sio wote UPUMZIKE KWA AMANI, Tilikupenda sana japo MUNGU amekupenda zaidi. AMEN




Chini; 
Watu mbali mbali wa rika zote, wanasiasa, wasanii, viongozi wa serikali na wananchi kwa ujumla walifika kwa majonzi makubwa kumuaga dada yetu hizi ni picha nilizofanikiwa kuzipiga katika tukio hili la kusikitisha tangu mwaka huu wa 2012 uanze;




Attached Thumbnails

Monday, January 16, 2012

MAREHEMU REGIA MTEMA: Wasifu, PICHA na Maelezo ya Ajali

Marehemu Regia Mtema
Wasifu wake Kwa Ufupi
Marehemu Regia Mtema alizaliwa Aprili 21, 1980. Alisoma elimu ya msingi kati ya mwaka 1989 na 1995. Alijiunga na Shule ya Sekondari Forodhani, Dar es Salaam mwaka 1996 hadi  1999 na kuhitimu kidato cha nne.  Aliendelea kidato cha tano 2002 na sita kati ya mwaka 2000 na 2002 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Machame, mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari


Mwaka 2003 hadi 2006 alisoma Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na kupata Shahada ya Maarifa ya nyumbani na Lishe. Baada ya kuhitimu shahada yake, marehemu Mtema alifanya kazi katika taasisi mbalimbali kabla ya kujiunga na Chadema na kuteuliwa kuwa Ofisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Vijana ya chama hicho.
Mwaka 2010 aligombea Ubunge katika Jimbo la Kilombero


Baadaye aliteuliwa kuwa Ofisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Mafunzo ya chama hicho, nafasi ambayo aliishikilia hadi mwaka 2010 alipoteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum.

Marehemu enzi za uhai wake akiwa
katika Viwanja vya Bunge Dodoma




Maelezo ya Ajali

Muonekano wa Mbele wa Gari alilokuwa akiliendesha Marehemu
Marehemu Regia alikuwa anaendesha gari aina ya Land Cruiser VX Limited (V8) lenye namba za Usajili T296 BSM. Ajali hiyo ilitokea mnamo saa 5:30 asubuhi katika maeneo ya karibu na Sekondari ya Ruvu. Ajali ilitokea pale Regia alipotaka kulipita gari lingine lililokuwa mbele yake na ghafla aliona gari jingine likija mbele yake kwa kasi.
Muonekano wa Pembeni

Ili kuepusha kugongana na lile gari lingine uso kwa uso alikwepesha gari lake na ndipo liliacha njia na kupinduka. Watu wengine saba waliokuwa naye kwenye gari hilo walilokuwa wakisafiria kuelekea Morogoro walijeruhiwa tu.
...
*************************************************************************
R.I.P REGIA ESTELATUS MTEMA
                                                                                                                   Na Solomon Lekui

   Pacha wa marehemu Regia mtema bi. Remjia mtema akiwa na gang gongo alilokuwa akilitumia marehemu pacha wake



PACHA wa Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Regia Mtema (32) aliyefariki juzi kwa ajali ya gari eneo la Ruvu mkoani Pwani, Remija Mtema (32) ameeleza alivyonusurika baada ya kushuka kwenye gari muda mfupi kabla ya ajali.

Akizungumza naTumaini habari  jana, Remija ambaye ni kurwa, alisema Regia kabla ya ajali iliyosababisha kifo chake, alikuwa akitoa kauli za kutia moyo na za kutarajia kuonana tena.

“Tulitoka nyumbani kwake Mbezi-Makabe, Dar es Salaam kwenye saa tatu asubuhi, mimi nilikuwa nakwenda Iringa na tuliondoka na gari lake hilo lililopata ajali nyumbani hapo, wakanishusha Mbezi stendi nisubiri basi la Iringa .

“Wakati tunatoka nyumbani alikuwa anaongea kwa uchangamfu sana, kwanza juzi (Ijumaa)
tulizungumza na kupanga kwamba mimi niende Iringa kuomba ruhusa kazini, maana kuna wakati nikiwa huru namsaidia kazi kama Katibu wake, tulipanga nikipewa ruhusa nirudi nimsaidie kwenye Kamati na Bungeni,” alisema Remija.

Kwa mujibu wa Remija, walikubaliana hivyo na baada ya kupanga mambo yao usiku huo wa
Ijumaa, walicheza sana karata.

“Ni karata za kuagana maana mimi ndio nilikuwa nasafiri kesho yake kwenda Iringa, asubuhi ndio tukaondoka huku tunacheka, mimi nikashukia Mbezi, alikuwa ni zaidi ya pacha wangu, alikuwa rafiki yangu,” alisema Remija.

Remija ambaye ni Ofisa Tarafa wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, alisema aliposhuka Mbezi
kusubiri gari, walikaa nae na watu wengine kwenye gari kwa karibu saa moja wakimsubiri mama yao, Bernadeta aliyekuwa akitokea Tabata-Chang’ombe nyumbani kwao.

“Mama alipofika aliingia garini na wakaondoka, pacha akasisitiza nikipata usafiri niwaambie, ni
kama alitamani niendelee nao lakini haikuwa hivyo, baada ya muda wa nusu saa mama alipiga simu kuniuliza kama nimepata basi maana waliona basi la Upendo limewapita, nikamjibu bado, baada ya muda mfupi nikapata basi la Budget,”

“Nilipoingia kwenye basi saa tano asubuhi hivi, nikamtumia ujumbe Regia kuwa nimepata basi, lakini ujumbe haukujibiwa, nikajua labda kwa kuwa alikuwa anaendesha gari, nikaendelea kusoma gazeti na tulipofika Ruvu niliona watu lakini sikutilia maanani nikaendelea kusoma gazeti,” alisema Remija.

Alisema kabla hajafika Chalinze, alipigiwa simu na mama yake kuwa wamepata ajali na
wapo Hospitali ya Tumbi na kumuomba dereva ashuke kwa kuwa ndugu zake wamepata ajali
Ruvu.

“Dereva na kondakta waliniuliza aina ya gari, nikawaambia wakathibitisha waliiona. akasimamisha gari nikashuka na kuanza safari ya kurudi hadi Hospitali ya Tumbi, nikakuta kweli Regia amefariki,” alisema Remija.

Alisema pacha wake alikuwa jasiri ambaye akiamua jambo lake ni lazima alifanye, alikuwa na huruma asiyependa mtu aonewe na alimuamini Mungu kwa kila jambo kutokana na malezi ya kiimani waliyopata kwa baba na mama yao mlezi.

Kwa mujibu wa Remija, yeye na pacha mwenzake walizaliwa Hospitali ya Ocean Road, jijini Dar
es Salaam Aprili 21 mwaka 1980, alikuwa mpenzi na shabiki wa timu ya mpira wa miguu ya Simba kwa hapa nchini na kwa nje alikuwa akipenda kufuatilia Barcelona ilipocheza zaidi ya timu nyingine.

Baba wa marehemu, Estelatus Mtema aliliambia gazeti hili jana kuwa anamshukuru Mungu kwa
kila jambo na kuomba majeruhi akiwemo mkewe waliolazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili walikohamishiwa wakitokea Tumbi juzi jioni, wapone mapema.

Utaratibu wa maziko

Mtema alisema misa itafanyika leo saa tisa alasiri katika Kanisa Katoliki la Segerea pamoja na heshima za mwisho na kesho kutakuwa na heshima za mwisho katika ukumbi wa Karimjee.

Alisema bada ya hapo safari ya kulekea Ifarakara itaanza na maziko yatakuwa Jumatano huko
Ifarakara mjini nyumbani kwa wazazi wa marehemu.

Majeruhi Muhimbili
Mtoto wa binamu wa mama wa marehemu, Theresia Simon, ambaye ilidaiwa kuwa amefariki
kutokana na kujeruhiwa vibaya kichwani, anaendelea vizuri alikolazwa wodi namba 10 Kibasila.

Theresia katika mahojiano, alisema anamshukuru Mungu hali yake inaendelea vizuri na maumivu yamepungua.

Baadhi ya vyombo vya habari jana, viliripoti kuwa Theresia aliyejeruhiwa kichwani, alikufa hivyo kufanya idadi ya walioaga dunia kuwa wawili akiwemo Mbunge Mtema.

Shangazi yake, Consolata Mwandenga alisema pia kuwa alimpa uji jana na kula vizuri asubuhi na mchana hivyo hali yake ni njema. Pia mama wa marehemu, Bernadeta na watu wengine
wawili, wanaendelea vizuri na wote wamelazwa katika wodi hiyo.

Vikao vya dharura Chadema
Wakati huo huo Sekretarieti ya Chadema jana ilifanya kikao cha dharura chini ya Uenyekiti wa Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa kupanga utaratibu wa chama na viongozi wake wakuu, kushiriki kikamilifu kwenye maombolezo, heshima za mwisho na hatimaye maziko yaliyopangwa kufanyika Ifakara.

Shughuli hizo za mazishi ya heshima kwa Mbunge huyo, kwa mujibu wa taarifa za Chadema, zitaongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe.

Mbali na Sekretarieti, pia Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa Chadema, ilifanya kikao cha
dharura, kwa kuzingatia uzito wa msiba uliotokea na kupitisha azimio kwamba wabunge wote wa Chadema washiriki kutoa heshima ya mwisho.

Kwa mujibu wa azimio hilo, wabunge wote wa chama hicho watasindikiza mwili wa Regia
hadi Ifakara na kushiriki maziko.
                                                                                                            Na SOLOMON LEKUI