Sunday, July 22, 2012
Tatizo la Maji litaisha lini?
Na. Hatibu jumbe
Ni miaka
hamsini sasa tangu Tanzania ijipatie uhuru wake toka kwa wakolon,kwa lengo la
kujiendeshea maisha yao wenyewe.Katika kipindi chote hicho bado suala la
upatikanaji wa maji safi na salama limekuwa likisuasua hasa kwa wakazi wa
vijijini.
Suala la
upatikanaji wa maji limekuwa ni tatizo sugu la licha ya kuwepo kwa sera na
kaulimbiu mbalimbali zinazo tolewa kila mwaka zikiwa na dhumuni la kuboresha na
kurekebisha upatikanaji wa maji mijini na vijijini.
Si ajabu
kuona misururu ya ndoo kwenye mabomba au watu na mikokoten yao
kueleke bombani katika miji kadhaa hapo Tanzania. Imesha wahi kuriportiwa
kupitia vyombo kadhaa vya habari kuwa mikioa ya Morogoro, Dodoma, Singida na baadhi ya maeneo ya Dar es
sallam kukabiliwa na adha ya maji katika misimu mbalimbali ya majira.
Mara nyingi
wahanga wakubwa wa janga hili ni wanawake ambao huwajibika kutafuta maji toka
pale yanapopatikana mpaka nyumbani, ambapo maranyingi huyatoa umbali mrefu.
Hali hii inakwamisha juhudi nzima ya maendeleo kwani badala ya watu kujumuika
katika shughuli nyingine za kimaendeleo wanaishia kupanga misururu na foleni
katika mabomba ya maji na vyanzo mbalimbali vya maji.
Maadhimisho
ya wiki ya maji mwaka huu kitaifa yamefanyika mkoani Iringa yakiwa na kaulimbiu
inayosema “Maji kwa Usalama wa Chakula”
Mipango ya
utekelezaji ya Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira iliyozinduliwa na rais
Jakaya Kiwete mwaka 2007, ililenga kuongeza upatikanaji wa huduma za majisafi
na salama katika miji mikuu 19 ya mikoa (ukiacha Dar es Salaam na Pwani) kutoka
asilimia 78 mwaka 2006 hadi asilimia 90 mwezi Desemba mwaka 2010. Hadi
ilipofika Desemba 2011, hali ya upatikanaji wa huduma za maji safi na salama
katika miji hiyo ilikuwa asilimia 88 ambapo lengo halikufanikiwa kwa asilimia 2
Katika
maeneo ya vijijini, lengo lilikuwa kuongeza Desemba mwaka 2006 hadi asilimia 65
ifikapo mwezi Desemba 2010. Hadi Desemba 2011, upatikanaji wa huduma za maji
vijijini ulikuwa katika wastani wa asilimia 58, ikiashiria kuhitajika kwa
juhudi za ziada ili tuweze kufikia lengo. Juhudi hizo za ziada ni pamoja na zile
zinazohitajika kutekelezwa ili kuboresha huduma za maji katika Jiji la Dar es
Salaam, katika miji mikuu ya wilaya na miji midogo.
Licha ya
juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali na mashirika binafsi katika kutatua
tatizo hili la maji ni kama mradi wa visima vijijini, dhahir kuwa juhudi hizo
zimegonga mwamba kwani wananchi waliowengi wanakabiliwa na tatizo hili.
Hakuna asiye
tambua kuwa ukosefu wa maji huweza
kuhatarisha maisha ya binadadamu na hata kupelekea kifo kwani maradhi
mbalimbali ya milipuko huibuka kama kipindupindu kutokakana na kunywa maji
yasiyo safi na salama.
Kwa namna
moja ama nyingine wananchi wanahusika moja kwa moja katika kufaya rasilimali ya
maji kupotea kwa kulima kando kando ya vyanzo vya maji au kukata miti.
Wote
tumeshaona kile kinacho tokea Somalia jinsi watu na mifugo inavyoteketea kwa
ukosefu wa maji. Takwimu zinasema kwamba
kutakuwa na ukosekanaji wa maji ifikapo mwaka 2025 endapo vyanzo vya maji
vilivyopo sasa havitotunzwa.
Miradi
mbalimbali imekuwa ikianzishwa kama vile za kilimo cha umwagiliaji, ufugaji
huku sekta hizi zote zikiwa na vikwazo vikubwa vya ukosekanaji wa maji ya
kutosha.
Hatunabudi
wananchi tuunge mkono juhudi zinazofanywa na serikali juu ya upatikanaji wa
maji safi na salama ikiwemo kutunza vyanzo vya maji na kuwafichua waharibifu wa
vyanzo hivyo, pia tuache tabia ya kupasua mabomba ya maji.
Subscribe to:
Posts (Atom)