Sunday, January 27, 2013

MANGULA AWALAMBISHA FAITH CHOIR MILIONI 15

Na Solomon Lekui

Makamu mwenyekiti wa CCM taifa ndugu Philip Mangula akiongozwa na mwenyekiti wa bodi ya Chuo kikuu cha Tumaini kuingia katika ukumbi wa Multipurpose kwa ajili ya kuchangia kwaya ya faith ya CCT kwa ajili ya kurekodi mkanda wa Video wa nyimbo za injili


mgeni rasmi akiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa iringa ndugu Jesca msambatavangu (kushoto) na mbunge wa viti maalum ndugu rita kabati na viongozi wengine wa CCM wilaya na mkoa


waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi wa Tumaini Nelly Henericus naye alikuwepo kwa ajili ya kuinua kazi ya Mungu


DPAA Dr. Richard Lubawa pamoja na DPA Dr.. Chachage wakiwa katika harambee hiyo kwa ajili ya kuichangia kwaya ya Faith CCT chuoni Tumaini


wanakwaya wakiingia jukwaani kwa mbwembwe. Utaipenda


kinadada nao hawapo nyuma kwa mapozi na tabasamu murua kabisa


kama ni dereva wa gari basi ndio huyu ambaye ni dereva (mwalimu) wa kwaya ya Faith CCT katika chuo kikuu cha Tumaini


Faith wakifanya mambo jukwaani


wageni wakitazama kwa tabasamu na furaha kwaya ya Faith wakifanya vitu vyao jukwaani


Sololist hao!!!!


Mwenyekiti wa bodi ya chuo kikuu cha Tumaini Dr. Owdenburg Mdegela ambaye pia ni askofu wa dayosisi ya Iringa akimkaribisha mgeni rasmi katika harambe hiyo


Mgeni rasmi akiwahutubia wageni waliokuwepo katika harambee hiyo


karibu mwanakwaya mwenzangu!!!! Hivyo ndivyo askofu alivyomkaribisha mgeni rasmi kuhutubia na kuchangia kwaya tayari kwa ajili ya kurekodi


Katibu wa kwaya akisoma risala fupi kwa mgeni rasmi


baada ya harambe ni hoihoi vifijo na nderemo. utaipenda tu
Makamu mwenyekiti wa CCM taifa ndugu Philip Mangula, ameongoza harambee ya kuchangia kwaya ya Faith ya CCT ya chuo kikuu cha Tumaini fedha kwa ajili ya kurekodi nyimbo zao za injili za video. Mangula aliwaambia wanakwaya kuwa alikuwa mwimbaji wa kwaya akiwa kijana na walikuwa wakitumia chombo cha kitamaduni kiitwacho Mangala kwa ajili ya kumsifu mungu wao wakiwa pamoja na askofu Mdegella

katika ukumbi huo wa Multiurpose Mangula aliwaambia washiriki kuwa ameingia kwenye siasa pasipo kusudio baada ya kuitwa na REO mwaka 1966 ili akasomee uongozi katika chuo cha uongozi kivukoni baada ya aliyechaguliwa kwenda kusoma chuo hicho kuuguliwa,ndipo alipoteuliwa kwenda kusoma hapo. Mangula alipamba ukumbi kwa kuimba wimbo wa  "Tumshukuru mungu" wimbo ambao ulipokewa kwa shangwe na waliohudhuria hapo


Katika harambee hiyo iliyojawa na viongozi wa CCM wa ngazi mbalimbali, Mh. Mangula alichangia shilingi milioni Tano,watoto wake walichangia laki saba na wadau mbalimbali wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa ndugu Jesca Msambatavangu aliyechangia shilingi laki tano.


Takriban shilingi milioni 15 zilipatikana katika harambee hiyo ambayo mbunge wa kalenga Mh. Mgimwa amechangia milioni tano huku mwenyekiti wa CCM mkoa akisisitiza wote walioahidi kuwasilisha michango yao ndani ya wiki moja kupitia namba 0758804479


Mangula amekuwa mkuu wa wilaya kwa miaka sita, mkuu wa mkoa kwa mikoa tofauti kwa miaka saba, katibu mkuu wa CCM kwa miaka kumi na sasa makamu mwenyekiti wa CCM bara kwa miaka mitano hadi 2017 atakapokabidhi kijiti kwa wengine


MUNGU IBARIKI TUMAINI UNIVERSITY

MUNGU IBARIKI FAITH CHOIR
MUNGU IBARIKI CCT