Friday, November 11, 2011

Let’s observe patriotism to lift up our development

Its fifty years since our county achieved independence from German. On 9, December 1961, Tanzania under the leadership of the late Mwl. Julius Nyerere became an independent country. The problem remained was un­derdevelopment, this was a result of colonial legacy to not only Tanzania but also other African countries.
We still have the challenge of lacking enough capital to run our schemes including agricultural schemes, but this should not discourage us with our mission in growing our economy. What we need is to know the ob­stacles of the development.
The illiteracy class is the one which is in a position to bring changes to the country. The most important things for the development of any county are accountability and patriotism. We as the educated class need to have love and respect to our country. These two, in the combination with personal morality will make the civil servants and the leaders to behave in accountability manner.
The dishonest practices like scam and corruption are the great enemies of our country’s economy. Many corruption cases have been experienced in our country; these are those which including the prominent leaders who are expected to mobilize strategic plans for sustained development.
We Tumaini University, the educational institution also have the great role to bring changes in our society as well as the whole nation. As we participated in the fifth independence exhibition in Iringa region, we need to make sure we bring positive changes in our society.
Tumaini University extends its branches and accredits its colleges to University status. This is very beneficial thing to the students, the staff and the whole country at large as it widens the chance to the people to attain high education.
The incensement of the educated people should also rise simultaneously with the spirit of patriotism to our societies and the country as well. Tu­maini University and its branches are therefore supposed to prepare the future leaders who will effectively be responsible to bring development to our country.
We believe that Tumaini is one of the universities in Tanzania that shapes the students to be good future leaders, but still there is a need to shape them in more patriotic manner. This will contribute to the termina­tion of the scam and dishonest in the government and its system as well.

Thursday, November 10, 2011

Serikali haijatoa suluhisho la kudumu migomo elimu ya juu.






Na John Alex.

Malalamiko yanayoendelea kutolewa na wanafunzi wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini ni dalili sio tu ya   wasomi hao kutokuridhishwa na hatua  zinazochukuliwa na serikali  katika kutatua changamoto  zinazowakabili  lakini pia  kushindwa vikali kwa serikali  iliyoko madarakani katika utekelezaji wa sera  zake kuhusu elimu  ya juu nchini.

Wote mtakubaliana na mimi kuwa wasomi wa vyuo vikuu nchini ni hazina kubwa sana kwa taifa la Tanzania  kwani hao ndio chimbuko la mawazo mapya na uelewa na  pia ni chazo  kikubwa sana cha maendeleo ya taifa. letu kwani  taifa bila wasomi ni sawa na  Gari  kubwa la mkaa litembealo njiani usiku bila  taa wakati wowote laweza gonga mti  au mwamba na kupinduka..

Matatizo yanayowakabili wanafunzi wasomi wa vyuo vikuu nchini  ni mengi  lakini leo nataka nizungumzie moja tu ambalo limekuwa changamoto kubwa  sana  kwa wasomi hawa  wa vyuo vikuu  na bado litaendelea kuwa changamoto yenye kuleta madhara makubwa  endapo serikali na mamlaka husika hazitawajibika ipasavyo kutafuta ufumbuzi na kulitatua kabisa tatizo hilo.

Swala la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini  limezua mjadala mzito sana  kwa wanafunzi  kwani  wasomi hao wamekuwa wakiiomba serikali iongeze fedha  za  mikopo  hususan fedha za kujkiimu wawapo vyuoni na pia  ada ikibidi..Kilio hiki cha wanachuo ni cha muda mrefu sana. na wengi   wamepoteza  masomo  kutokana na kushindwa kujikimu wenyewe kutokana na ugumu wa maisha  ambao kimsingi husababishwa na kupanda kwa gharama  za maisha .Bei ya bidhaa nchini inapanda kila kukicha na hivyo hata taasisi binafsi za elimu  zote pia inawalazimu kupandisha gharama za utoaji huduma.

Baada ya kilio cha muda mrefu  cha wasomi hawa kilichoambatana na  maandamano  na migomo kila kukicha serikali ikaanza walau kulifikiria na kuliangalia upya swala la mikopo na hatimaye kukiri kuwa  ni kweli ghrama za  maidha ya sasa si sawa na  kiwango cha fedha za kujikimu walichokuwa wanatoa  hadi hivi karibuni..Fedha ya kujikimu ya  mwanafunzi mmoja kwa siku ilikuwa ni shilingi za kitanzania elfu tano tu.Hivyo serikali kwa kuliona hilo,ikaamua kupandisha kiasi cha fedha hizo kutoka  shilingi elfu tano hadi elfu saba na  mia tano kwa siku ambapo imeongezeka  shilingi elfu mbili na mia tano tu ambayo imeanza kulipwa rasmi mwaka huu  wa masomo.

Hata hivyo  ongezelo la kutoka  shilingi elfu tano kwa siku hadi elfu  saba na mia tano halikuwa makubaliano kati  ya wanafunzi wa vyuo vikuu  kote nchini na serikali bali wasomi hao waliiomba serikali  kutokana na kupanda kwa gharama za maisha ongezeko la kutoka elfu tano hadi elfu kumi kwa siku.Hapa tunaona kuwa serikali haijatekeleza  wala  haijatoa suluhu bali imefanya kwa sehemu  tu kitu ambacho hakijawaridhisha wasomi hawa hata kidogo na ndio maana hata makala  za kuipongeza serikali  kwa utekelezaji huo hakuna!

Pamoja na kukubaliana na hali halisi ili kutopoteza wakati,wanafunzi wasomi  hawa wote wameamua kujikalia kimya huku wakijiliwaza  na kauli za wahenga kama vile, mvumiivu hula mbivu,na kwa ahadi za  seikali za tutafanya, basi wasomi hawa pia wanarejea  kwenye  kauli za wahenga kuwa  subira yavuta kheri.

Sasa tayari wanafunzi hawa wako vyuoni,  lakini badala ya kupungua maumivu ndio kwanza yameongezeka.Mamlaka iliyokabidhiwa dhamana ya  kushughulikia pesa za wanafunzi  ziwafikie kwa wakati yani Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu,(HSLB) inaonyesha kushindwa  kabisa kutekeleza jukumu lake,hali inayofunua hisia mpya kuwa kuna urasimu mkubwa ndani  ya chombo hicho cha serikali ambacho chenyewe pia kinatupa lawama kwa serikali  kwamba hatujapokea pesa kutoka serikalini.

Kutokana na kutokuwajibika kwa bodi ya mikopo na urasimu uliopo pamoja na rushwa iliyokithiri, serikali kutolichukulia uzito swala hili,madhara makubwa yanaendelea  kutokea,  ambapo mwaka huu takribani wanafunzi wapatao elfu kumi na nne wamekosa mkopo je watakwenda wapi wale watoto wa wakulima?

Kumeundwa bodi ndogo za mikopo vyuoni na serikali imetoa tamko kuwa  fedha za mikopo zitapelekwa vyuoni jambo ambalo ni kukiuka mkataba kati ya bodi ya mikopo na wanafunzi wanaoendelea  na  masomo kwa mwaka wa pili na kuendelea  kwa sababu  haukuwa hivyo.Fedha zilitakiwa zipelekwe  moja kwa moja kwenye akaunti za  wanafunzi wenyewe ili kuondoa  walau kwa sehemu tatizo la  ucheleweshaji wa fedha za kujikimu na ada kwa wanachuo hawa kwani baadhi ya vyuo wamekuwa wakichelewesha sana fedha za  kujikimu kwa wanafunzi.

Kumeibuka  hisia miongoni mwa wanafunzi wa baadhi ya vyuo  hapa nchini kuwa kuna vyuo  vikuu vinavyopewa kipaumbele  aidha kwa kuviogopa  au kwa namna yeyote ile ya kiupendeleo.Wasomi hawa wa wa vyuo baadhi wameilaumu mamlaka husika kwa kuchelewesha  fedha za vyuo vyao huku  huku wakihoji kwanini  vyuo vingine vipewe fedha kwa wakati na vingine visipewe kwa wakati?

Ni dhahiri kuwa serikali  kutokana  na kutojali na kutokulipa kipaumbele  swala  hili inashusha kiwango cha elimu nchini kwani migomo itaendelea kila kukicha na ndio maana hatukosei kabisa kusema kuwa  serikali itegemee migomo zaidi kwani  tatizo linazidi kuwa kubwa a badala ya kupungua.

Serikali haina budi  kulitizama upya  swala hili na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu kama inavyohangaika na kuimarisha miundombinu ya barabara kuu nchini ambapo kwa kweli inafanya vizuri sana huko.

Aidha serikali   haina budi kuiwajibisha menejimenti ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini na kuhakikisha kuwa  inaunda menejimenti madhubuti ambayo itafasnya kazi  kwa umakini  mkubwa na kwa haki huku mamlaka iliyokabidhiwa dhamana ya kuzuia  na kupambana na rushwa  ikiwa karibu kabisa na hivyo kuzuia urasimu na rushwa ambayo kimsingi ndio chanzo  cha matatizo.

                                                                     John Alex Mganga-0658385435

                                                                    E.mail-Johnmganga@yahoo.com.
                                                                            














Naibu waziri wa mikopo aapishwa katika chuo kikuu cha Tumaini Iringa.



Raisi wa chuo kikuu cha Tumaini Iringa Mh. Method Kagoma
akiwa anaelezea jambo wakati wa sherehe  ya kuapishwa naibu waziri wa mikopo.
Moses Samson alipokuwa akiapishwa katika ofisi ya raisi
kama naibu waziri wa mikopo katika chuo  cha Tumaini  Iringa.
                                    

Naibu waziri mteule akiwa anasikiliza nasaha za raisi wa chuo.
Spika wa bunge la serikali ya wanafunzi Henry Mwinuka(kushoto),naibu spika  Mauna  Chuma(katikati)
wakiwa  na waziri  wa ulinzi Eliasa Salumu katika sherehe hiyo fupi ya kumuapisha naibu waziri wa mikopo.
                                               
Waziri mkuu wa chuo cha Tumaini Iringa, Bahati Richardson
akiwa  anaongea machache  baada ya  kuapishwa  kwa  Moses Samson.

Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo katika sherehe ya kuapishwa
naibu waziri  wa mikopo  ndani ya ofisi  ya raisi.

                                  Posted by Frank Kimaro
                                         

MUSA MAHUNDI KOCHA MPYA WA MPIRA WA MIGUU TUMAINI IRINGA

 By Hija Mkali

Kocha wa zamani wa klabu ya Polisi Iringa,Lipuli pamoja na timu ya Mkoa wa Iringa (Mkwawa Horeos),Musa Mahundi,amewasili jana katika kiwanja cha mpira wa miguu cha chuo kikuu cha Tumaini Iringa.

Mahundi,ameteuliwa na chuo kwa ajili ya kuisaidia timu katika mashindano ya vyuo vikuu nchini (Shimivuta),ambayo yanatarajiwa kuanza mnamo terehe 26 mwezi huu katika kiwanja cha Mkwakwani jijini Tanga.

Aidha,mahundi,''aliomba ushirikiano baina yake na wachezaji ili kudumisha nidhamu,uadilifu ndani na na nje ya uwanja''.

Mahundi,''alianza kazi jana na kuangalia wachezaji atakao wafaa ili kwenda nao Tanga na kuleta ushindani mkubwa na kuweza kuleta heshima chuo (Tumaini Iringa)''.

Wakati huohuo,mlezi wa wanafunzi,mchungaji Oswald Ndelwa,aliwaomba wachezaji kumpa ushirikiano wa kutosha kocha (Mahundi),ili kukiletea heshima chuo chetu.

Kwa upande wake nahodha timu hiyo,George Kanji,aliwataka wachezaji wenzake kuleta mwamko baina yao.

Sanjari na kusema hivyo,ili soka la Tumaini,liendelee kuwepo na kukuwa hapana budi kuwepo kwa nidhamu,uadilifu na heshima baina yetu.

Programu ya mwalimu ni mpango ni muda mfupi wenye lengo la kuwajenga wachezaji kisaikolojia kwenye soka la ushindani,pia ani fursa ya kuona vipaji vipya vya wachezaji chipukizi na kutumia nafasi hiyo kuendeleza soka kwa faida ya badae.

HII NDIO SERIKALI YETU...

posted by Sixtus Bahati

Wednesday, November 9, 2011

MKESHA WA MWENGE WA UHURU MKOANI IRINGA......



Wakaazi wa mkoa wa Iringa na vitongoji vyake wakicheza muziki katika mkesha wa mwenge wa uhuru katika uwanja wa samora jana usiku(picha na Sixtus Bahati)

MWENGE WA UHURU WAWASILI MKOANI IRINGA.

Mwenge wa Uhuru ukiwa katika uwanja wa samora baada ya kuwasili mkoani Iringa.(picha na Sixtus Bahati)