Sunday, March 18, 2012

                                          Wachezaji wa mpira wa wavu wa Tumaini wakipeana
                                           moyo baada ya kupoteza mpira
                                          Wachezaji wa Tumaini wakiwa makini kumsikiliza
                                           refa wamchezo
                                           Mchezaji wa TEKU akiinuka mara baada ya kuanguka
                                           kulikotokana na kushindwa kuzuia smash ya mmoja wa
                                           wachezaji Tumaini
                                           Wachezaji wa TEKU wakiwa makini kurudisha mpira
                                            kwenye eneo la Tumaini

Friday, March 16, 2012

Maadhimisho ya wiki ya maji yaanza mkoani Iringa.

Na. Frank Kimaro

matukio katika picha
katika banda la AMREF mambo yalikua hivyo watu wakiangalia vitu mbalimbali katika maonesho.


Bomba lililotengenezwa maalumu kwa ajili ya maonesho hayo
 
Mawakala wa kampuni ya bia ya Serengeti wakiwa ndani ya bango lao.
 
Kikundi cha ngoma kikiwa kinatumbuiza katika maadhimisho hayo.



BAADA YA KUONEKANA KUWA RAISI ATAHUDHURIA KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SHEREHE HIZO UKARABATI WA BAADHI YA BARABARA UMEANZA KAMA INAVYOONEKANA KWENYE PICHA HAPO CHINI . SWALI LINAKUJA KWAMBA WALIKUWA WAPI KUKARABATI SIKU ZOTE INA MAANA PESA ZINATOLEWA NA SERIKALI KWA AJILI YA UJENZI WA BARABARA ILA HAZITUMIKI KAMA INAVYOPASWA.

Kipande cha barabara kinachotengenezwa maeneo ya  mshindo manispaa ya  Iringa baada ya kuonekana  raisi atazuru katika manispaa hiyo.

Monday, March 12, 2012

Uzinduzi wa kampeni za CCM arumeru

Na solomon ole lekui

Baada ya chama cha demokrasia na maendeleo kuzindua kampeni zake huko arumeru ya mashariki siku chache ilizopita, chama cha mapinduzi nacho kimezindua kampeni zake leo hii. Vyama hivyo viwili vimezindua kampeni hizo ikiwa ni nafasi ya kipekee kwao kuwanadi wagombea wa kiti cha ubunge kupitia vyama vyao baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo solomon sumari kuaga dunia miezi michache iliyopita.

wakiongeaa kwa mbwembwe na bashasha, wabunge na viongozi wa CCM wameapa kushinda katika uchaguzi huo kwani CCM ni chama kilichokomaa na chenye sera nzuri.

Mabasi mengi yalionekana yakiingia kutoka sehemu mbalimbali kama engereyan,ngabobok na maeneo ya mbali ya jimbo hilo kuja kushuhudia uzinduzi huo. Aliyeandalia kuzindua kameni hizo ni rais wa awamu ya tatu mh. mkapa a.k.a Mr. clean


Mh. john komba

Basi la kampuni ya URIO safaris lililokuwa likiwatoa watu kutoka maeneo mbalimbali ya Arumeru kuja kushuhudia uzinduzi wa kampeni za CCM



wapenzi na wakereketwa wa CCM wakisubiri kwa hamu uzinduzi wa kampeni za chama chao



HATA WACHEZA TAARABU WALIKUWEPO



Picha zote kwa hisani ya http://www.mjengwablog.com/

Sunday, March 11, 2012

Uzinduzi wa chadema katika picha

Na solomon ole lekui

Name:  IMG_5170.JPG
Views: 0
Size:  3.68 MB


Name:  IMG_5157.JPG
Views: 0
Size:  3.50 MB


Name:  IMG_5154.JPG
Views: 0
Size:  1.76 MB
Name:  IMG_5165.JPG
Views: 0
Size:  2.75 MB

Name:  IMG_5169.JPG
Views: 0
Size:  3.04 MB
Ni hoi hoi vifijo na nderemo katika viwanja vya shule ya msingi leganga iliyoko USA river mkoani Arusha pale chama cha demokrasia na maendeleo walipozindua kampeni zao za uchaguzi mdogo katika jimbo la Arumeru mashariki. Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kufariki kwa kansa ya ubongo.
katika uchaguzi huo wagombea saba wametamba kushinda huku chama cha mapinduzi na chama cha demokrasia na maendeleo zikionekana kuwa na ushindani mkubwa zaidi.

Mgomo na msimamo wa madaktari ni mfano wa kuigwa kupambana na ahadi hewa za serikali

Na solomon ole lekui

Ukilitazama swala la sakata la mgomo wa madaktari juu juu unaweza kuwalaumu na kuwaita watu wasio na huruma na hawawatendei haki wagonjwa,wauaji,wasaliti,wamek iuka kiapo cha udaktari n.k. Kitu ambacho serikali JK na utawala kwa ujumla katika propaganda na porojo zao wanataka tuamini hivyo.

Ukilitazama kwa ndani,wakualaumiwa na kubeba lawama zote ni Mh.Rais JK,serikali na chama Tawala CCM kwa sababu zifuatazo JK katika uteuzi wa mawaziri na nafasi mbalimbali katika serikali na taasisi mbali mbali hazingatii uwezo,uzoefu na sifa za mchaguliwa bali uswaiba na masilahi katika makundi ndani ya chama tawala.

Hali ambayo inampa hali ngumu ya kutoa uamuzi wa kuwawajibisha wanapofanya ndivyo sivyo.Tatizo lingine kwa vile serikali na utawala hauna dhana ya kuwatumikia wananchi hivyo kauli nyini na ahadi wanazozitoa zinatoka katika ulimi na kubaki katika makaratasi bila kufanyiwa utekelezaji kwa maana ya kua za kisanii na porojo ili muda upite. Hakuna anaewajibika kwa kauli au ahadi serikali au JK inazozitoa kwa hali hii kutegemea ufanisi ni ndoto ya mwendawazimu.

Mambo mengi yametokea(ufisadi,rushwa,uzembe n.k) katika serikali na viongozi katika serikali na taasisi za serikali hakuna anayejiuzulu au kuwajibishwa tume baada ya tume imekwisha.Hata huko katika CCM viongozi wanaopatikana huko ni kwa njia ya rushwa na ufisadi ambapo hao ndio viongozi baadae katika serikali.

NENO KUJIUZULU KUWAJIBIKA KATIKA UTAWALA HUU HALIMO KATIKA MSAMIATI WAO.NJIA PEKEE YA KUWALAZIMISHA WAWAJIBIKE NI MIGOMO NA MANDAMANO HIVYO MGOMO WA MADAKTARI UMEONYESHA NJIA JINSI YA KUIBANA SERIKALI ITIMIZE AHADI ZAKE NA SIO POROJO.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Thursday, February 9, 2012

MAANDAMANO KUUNGA MKONO MADAKTARI YATAIFANYA SERIKALI ISIKIE?





Jana Dar es salaam
Picha kwa hisani ya Michuzijr
POSTED BY SOLOMON OLE LEKUI 


PINDA ANATAKA KUKUTANA NA MADAKTARI

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA YUPO DAR ES SALAAM KUTOKA DODOMA KUSHUGHULIKIA MGOMO WA MADAKTARI AMBAO UMEKUWA UKIENDELEA KWA LENGO LA KUUPATIA UFUMBUZI. JANA AMEKUTANA NA UONGOZI WA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI PAMOJA NA MADAKTARI BINGWA KUTOKA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI NA WASTAAFU. LEO SAA 3 ASUBUHI ATAKUTANA NA MADAKTARI BINGWA, MADAKTARI WALIOSAJILIWA (REGISTRALS) NA MADAKTARI WALIOKO KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO (INTERNS) NA BAADA YA HAPO SAA 4 ATAKUTANA NA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA MUHIMBILI, MOI, OCEAN ROAD NA WAWAKILISHI KUTOKA HOSPITALI ZA MKOA WA DAR ES SALAAM, KWENYE UKUMBI WA CPL, MUHIMBILI. MATARAJIO YA SERIKALI NI KWAMBA MAZUNGUMZO HAYO YATAWEZA KUMALIZA MGOGORO HUU NA MADAKTARI WOTE KUREJEA KAZINI NA HIVYO KUREJESHA HUDUMA ZA MATIBABU KATIKA HALI YA KAWAIDA KWA WANANCHI WA TANZANIA. HIVYO SERIKALI INAWAOMBA WOTE WANAOHUSIKA WAFIKE KATIKA MIKUTANO HIYO BILA YA KUKOSA. (IMETOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
POSTED BY SOLOMON OLE LEKUI 


MAANDAMANO YA MGOMO WA MADAKTARI YATAWANYWA NA POLISI




Makubaliano: Tukutane Salander Bridge mchana huu (saa nane); tuwe na mabango ili kuishinikiza serikali kuacha kufanya mzaha na afya za watu.Tujitokeze kwa wingi; tutakubaliana zaidi cha kufanya baada ya hapo."Source:
Legal and Human Rights Centre | Facebook
POSTED BY SOLOMON LEKUI