Monday, March 19, 2012
Sunday, March 18, 2012
Wachezaji wa mpira wa wavu wa Tumaini wakipeana
moyo baada ya kupoteza mpira
Wachezaji wa Tumaini wakiwa makini kumsikiliza
refa wamchezo
Mchezaji wa TEKU akiinuka mara baada ya kuanguka
kulikotokana na kushindwa kuzuia smash ya mmoja wa
wachezaji Tumaini
Wachezaji wa TEKU wakiwa makini kurudisha mpira
kwenye eneo la Tumaini
moyo baada ya kupoteza mpira
Wachezaji wa Tumaini wakiwa makini kumsikiliza
refa wamchezo
Mchezaji wa TEKU akiinuka mara baada ya kuanguka
kulikotokana na kushindwa kuzuia smash ya mmoja wa
wachezaji Tumaini
Wachezaji wa TEKU wakiwa makini kurudisha mpira
kwenye eneo la Tumaini
Saturday, March 17, 2012
Friday, March 16, 2012
Maadhimisho ya wiki ya maji yaanza mkoani Iringa.
Na. Frank Kimaro
matukio katika picha
| katika banda la AMREF mambo yalikua hivyo watu wakiangalia vitu mbalimbali katika maonesho. |
| Bomba lililotengenezwa maalumu kwa ajili ya maonesho hayo |
| Mawakala wa kampuni ya bia ya Serengeti wakiwa ndani ya bango lao. |
| Kipande cha barabara kinachotengenezwa maeneo ya mshindo manispaa ya Iringa baada ya kuonekana raisi atazuru katika manispaa hiyo. |
Monday, March 12, 2012
Uzinduzi wa kampeni za CCM arumeru
Na solomon ole lekui
Baada ya chama cha demokrasia na maendeleo kuzindua kampeni zake huko arumeru ya mashariki siku chache ilizopita, chama cha mapinduzi nacho kimezindua kampeni zake leo hii. Vyama hivyo viwili vimezindua kampeni hizo ikiwa ni nafasi ya kipekee kwao kuwanadi wagombea wa kiti cha ubunge kupitia vyama vyao baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo solomon sumari kuaga dunia miezi michache iliyopita.
wakiongeaa kwa mbwembwe na bashasha, wabunge na viongozi wa CCM wameapa kushinda katika uchaguzi huo kwani CCM ni chama kilichokomaa na chenye sera nzuri.
Mabasi mengi yalionekana yakiingia kutoka sehemu mbalimbali kama engereyan,ngabobok na maeneo ya mbali ya jimbo hilo kuja kushuhudia uzinduzi huo. Aliyeandalia kuzindua kameni hizo ni rais wa awamu ya tatu mh. mkapa a.k.a Mr. clean
Mh. john komba
Basi la kampuni ya URIO safaris lililokuwa likiwatoa watu kutoka maeneo mbalimbali ya Arumeru kuja kushuhudia uzinduzi wa kampeni za CCM
wapenzi na wakereketwa wa CCM wakisubiri kwa hamu uzinduzi wa kampeni za chama chao
HATA WACHEZA TAARABU WALIKUWEPO
Picha zote kwa hisani ya http://www.mjengwablog.com/
Sunday, March 11, 2012
Uzinduzi wa chadema katika picha
Na solomon ole lekui
Ni hoi hoi vifijo na nderemo katika viwanja vya shule ya msingi leganga iliyoko USA river mkoani Arusha pale chama cha demokrasia na maendeleo walipozindua kampeni zao za uchaguzi mdogo katika jimbo la Arumeru mashariki. Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kufariki kwa kansa ya ubongo.
katika uchaguzi huo wagombea saba wametamba kushinda huku chama cha mapinduzi na chama cha demokrasia na maendeleo zikionekana kuwa na ushindani mkubwa zaidi.
Mgomo na msimamo wa madaktari ni mfano wa kuigwa kupambana na ahadi hewa za serikali
Na solomon ole lekui
Ukilitazama swala la sakata la mgomo wa madaktari juu juu unaweza kuwalaumu na kuwaita watu wasio na huruma na hawawatendei haki wagonjwa,wauaji,wasaliti,wamek iuka kiapo cha udaktari n.k. Kitu ambacho serikali JK na utawala kwa ujumla katika propaganda na porojo zao wanataka tuamini hivyo.
Ukilitazama kwa ndani,wakualaumiwa na kubeba lawama zote ni Mh.Rais JK,serikali na chama Tawala CCM kwa sababu zifuatazo JK katika uteuzi wa mawaziri na nafasi mbalimbali katika serikali na taasisi mbali mbali hazingatii uwezo,uzoefu na sifa za mchaguliwa bali uswaiba na masilahi katika makundi ndani ya chama tawala.
Hali ambayo inampa hali ngumu ya kutoa uamuzi wa kuwawajibisha wanapofanya ndivyo sivyo.Tatizo lingine kwa vile serikali na utawala hauna dhana ya kuwatumikia wananchi hivyo kauli nyini na ahadi wanazozitoa zinatoka katika ulimi na kubaki katika makaratasi bila kufanyiwa utekelezaji kwa maana ya kua za kisanii na porojo ili muda upite. Hakuna anaewajibika kwa kauli au ahadi serikali au JK inazozitoa kwa hali hii kutegemea ufanisi ni ndoto ya mwendawazimu.
Mambo mengi yametokea(ufisadi,rushwa,uzembe n.k) katika serikali na viongozi katika serikali na taasisi za serikali hakuna anayejiuzulu au kuwajibishwa tume baada ya tume imekwisha.Hata huko katika CCM viongozi wanaopatikana huko ni kwa njia ya rushwa na ufisadi ambapo hao ndio viongozi baadae katika serikali.
NENO KUJIUZULU KUWAJIBIKA KATIKA UTAWALA HUU HALIMO KATIKA MSAMIATI WAO.NJIA PEKEE YA KUWALAZIMISHA WAWAJIBIKE NI MIGOMO NA MANDAMANO HIVYO MGOMO WA MADAKTARI UMEONYESHA NJIA JINSI YA KUIBANA SERIKALI ITIMIZE AHADI ZAKE NA SIO POROJO.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Subscribe to:
Posts (Atom)








