Tuesday, January 31, 2012

Twiga Starz yaikandamiza timu ya TaIifa YA Namibia 5-2

Wachezaji wa timu ya wanawake Twiga starz wakishangilia

Mwanahamisi Omari Gaucho akiruka daruga la wachezaji wa Namibia

Kikosi cha Twiga starz

Asha Rashidi Mwalala akipiga shuti kuelekea golini mwa Namibia


Posted by Hija Mkali

Friday, January 27, 2012

Mh. John Mnyika aungana na madaktari

Na Frank Kimaro
                                            Waraka wa mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Myika

 Mgomo wa madaktari unaoendelea hivi sasa umedhihirisha kwamba tuna serikali dhaifu yenye ombwe la uongozi. Haiwezekani wananchi wakawa wanakufa kwa kukosa matibabu stahiki na wengine wakipata madhara kutokana na kuchelewa kupata matibabu sababu ya mgomo wa madaktari halafu viongozi wenye dhamana hawachukui hatua sahihi.
Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye mwenye dhamana kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 33 ndiye kiongozi wa shughuli za serikali na ibara ya 35 shughuli zote za utendaji wa serikali zinatekelezwa na watumishi wa serikali kwa niaba ya Rais; ameondoka kwenda nje ya nchi mgomo ulipoanza na hakuna kauli yoyote mpaka sasa toka kwa Makamu wa Rais wala kwa Ikulu.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda badala ya kwenda kwenye eneo la mgomo na kuzungumza na madaktari naye ameishia kuzungumza na vyombo vya habari. Waziri wa Afya Dk. Haji Mponda na Naibu Waziri Dk. Lucy Nkya nao jana wamezungumza na waandishi wa habari badala ya kwenda kukutana na madaktari na kuzungumza nao kuhusu madai yao ya msingi.

Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika

Kwa upande wetu CHADEMA tulitoa kauli tarehe 25 Januari 2012 ya kutaka serikali ichukue hatua na tuliona tuipe serikali nafasi ifanye kazi yake hata hivyo serikali haionyeshi kuupa uzito unaostahili mgogoro huu wenye kuathiri hali za wagonjwa na maisha ya wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Tuliacha kwenda katika eneo la mgomo kukutana na madaktari katika siku za awali kuepusha suala hili kutafsiriwa kuwa ni la kisiasa. Hata hivyo, kuchelewa kwa serikali kukutana na madaktari kunahitaji hatua za pamoja. Dhamira yangu kama mwananchi, mbunge katika mkoa wa Dar es Salaam na kiongozi wa chama cha siasa naumizwa na hali inayoendelea. Ni vigumu kuweza kuendelea na majukumu ya kibunge na ya kichama katika masuala mengine wakati serikali iko legelege katika suala ambalo linahusu uhai wa wananchi wenzangu uko mashakani.

Hivyo nawajibika siku ya leo kuelekeza nguvu katika kuungana mkono na madaktari katika madai yao ili kuishinikiza serikali kuweza kutuma ujumbe mkubwa kukutana na madaktari leo au kesho. Na iwapo serikali haitakutana nao katika muda huo, itabidi uongozi wa kambi ya upinzani bungeni ukiwa ni serikali kivuli na uongozi mkuu wa CHADEMA ukiwa ni chama mbadala kuweza kukutana nao.

Natambua kwamba uzembe na ufisadi katika serikali kwenye sekta ya afya unaligharimu taifa na maisha ya wananchi. Hivyo, CHADEMA inaitaka serikali kukamilisha kwa haraka majadiliano na madaktari na kutimiza madai yao ili kuepusha madhara zaidi kwa umma.

Nawapa pole wananchi ambao wameathirika na migomo inayoendelea na kuzingatia kwamba mgomo huo umesababishwa na udhaifu katika serikali.

Natoa mwito kwa umma wa watanzania kuwaunga mkono madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya katika hospitali na zahanati za umma kama sehemu ya kuboresha huduma katika maeneo husika.

Madai ya madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya nchini yasiposhughulikiwa kwa wakati na kwa ukamilifu watumishi husika wanaweza wasiwe kwenye mgomo wa wazi kama ilivyo kwa baadhi ya hospitali na zahanati nchini lakini wataendelea na migomo baridi kwa kutoa huduma mbovu au kuacha kazi kwenye maeneo ya umma na wengine kwenda kufanya kazi nje ya nchi wakati kukiwa na uhaba wa watumishi nchini.

Aidha, pamoja na migomo inayoendelea, naendelea kutoa rai kwa madaktari na watumishi wengine wa umma kuhakikisha maisha ya wagonjwa walio katika hali ya hatari yanaokolewa.

Nimezungumza na viongozi wetu wakuu kuhusu suala hili na natoa mwito kwa wadau wote kuunganisha nguvu katika kuisimamia serikali kushughulikia madai ya madaktari na wafanyakazi wengine wa sekta ya afya kwa haraka ili kuepusha madhara zaidi kwa umma.

Wananchi wenzangu wa Jimbo la Ubungo na umma kwa ujumla uzingatie kwamba tangu Mwalimu Nyerere aondoke madarakani mwaka 1985, Serikali ya CCM imeongeza wingi wa majengo mbalimbali kwenye sekta ya afya hata hivyo imeshindwa kusimamia utoaji bora wa huduma za afya katika zahanati, hospitali na vituo vya afya. Kutokana na mfumo mbaya wa usimamizi wa sekta ya afya, misingi imara ya kuimarisha sekta ya afya iliyowekwa baada ya uhuru imevunjwa na kubomolewa ikiwemo katika masuala yanayohusu kujali maslahi ya watumishi wa umma katika sekta hii muhimu.

Hali hii imefanya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa na nakisi ya watumishi asilimia 48% na takwimu zinaonesha kuwa 18% ya wafamasia, 15% ya madaktari, 13% ya madaktari wasaidizi waliacha vituo vyao vya kazi na kwenda kutafuta kazi kwenye mashirika ambayo yanalipa mishahara mikubwa na mizuri. Nakisi hii itaongezeka zaidi iwapo madai ya msingi ya madaktari na watumishi wengine hayatashughulikiwa na serikali itaendelea kuchelewa kushughulikia migogoro na migomo mingine inayoendelea.

Ni imani yangu kwamba serikali ikiwa na dhamira inaweza kuongeza mishahara kwa watumishi wa sekta ya afya ili kuweza kuwavutia wataalamu kubakia nchini badala ya kwenda kugoma au kwenda kutafuta kazi nje ya nchi kutokana na malipo mazuri huko. Hii ni pamoja kuwezesha malipo ya mazingira magumu kutolewa kwa watumishi wa afya wanaofanya kazi katika maeneo na kada maalum.

Kwa sababu hii, leo sitashiriki kikao cha Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kinachoendelea ili kupata wasaa wa kufuatilia kwa karibu suala hili na kuwasiliana na viongozi wenzangu kwa ajili ya hatua zaidi za pamoja.

Monday, January 23, 2012

WAZIRI MKUU MHESHIMIWA MIZENGO PINDA ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TENKILOJIA CHA NELSON MANDELA MKOANI ARUSHA

  
                               Waziri mkuu mheshiwa  Mizengo Pinda akiwa na baadhi ya viongozi wakikagua  maendeleo ya ujenzi  wa chuo kikuu cha Nelson Mandela leo.          
                                                                                                             Na Consolata    Haule

Sunday, January 22, 2012

DK SLAA ANA KWA ANA NA RAIS KIKWETE IKULU.


Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa, Ikulu Dar es Salaam jana usiku katika muendelezo wa mazungumzo ya mchakato wa Katiba mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe na katikati ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Said Alfi. Picha na IKULU


RAIS Jakaya Kikwete amekutana na uongozi wa Chadema Ikulu Jijini Dar es Salaam, akiwemo Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa, kuzungumzia mchakato wa Katiba Mpya.Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili, mkutano huo ulifanyika jana kuanzia saa 10:30 jioni na kuendelea hadi usiku, lakini walifanya mapumziko mafupi saa tatu usiku.


Ujumbe wa Chadema uliokuwa wa watu wanane, ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe. Wengine waliofuatana naye pamoja na Dk Slaa ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, John Mnyika, Said Arfi, John Mrema, Profesa Mwesiga Baregu na Profesa Abdallah Safari. Hadi tunakwenda mitamboni kikao hicho kilikuwa kinaendelea.


Hii ni mara ya kwanza kwa Dk Slaa kukutana na Rais Kikwete tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2010, ambao Dk Slaa alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34 akiwa nyuma ya Rais Kikwete aliyepata kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17, Dk Slaa hakuwahi kukutana na mkuu huyo wa nchi ana kwa ana.
               
POSTED BY SIXTUS BAHATI.



ELIMU INA MAMBO!


POSTED BY SIXTUS BAHATI.

Saturday, January 21, 2012

BAJ WATANDAZA KANDANDA SAFI DHIDI YA MAENDELEO YA JAMII

Na Solomon Lekui
Full beki ya timu ya BAJ1 OLE LEKUI

Katika kuonesha kwamba timu ya wanafunzi wa Bachelor of Arts in Journalism kimejizatiti vizuri katika mpira wa miguu ( football) jana timu ya mwaka wa kwanza ilionesha kandanda la kitabuni baada ya kucheza pasi nyingi na safi zilizoifanya timu ya wapinzani wao BACD kuomba mechi kumalizika kabla ya wakati baada ya kuchoshwa na kandanda safi liloneshwa na vijana wa BAJ1. Mchezo huo ulianza kurindima kwenye mishale ya saa 11 na kumalizika saa moja kasoro.

Pamoja na kuonesha kandanda safi timu hizo zilitoka suluhu ya kufungana magoli 2-2 lakini mchezaji mmoja wa BACD aliumia vibaya sehemu za mbavu tukio lililopelekea kulazwa katika hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi.
Mashabiki nao hawajaachwa nyuma kwa kushangilia na kutia moyo huku wakiimba nyimbo za uhamasishaji kama vile "usiniumizieeeee....." watu weweeeeee                                      



wachezaji wa BAJ oscar,zephania pamoja na goalkeeper on duty waisaka chacha a.k.a "MURA"
Hawa ndio baadhi ya wachezaji wa timu ya BAJ kutoka kulia ni Oscar a.k.a mzee wa kiatu, katikati ni hija mkali a.k.a panya buku na ole lekui a.ka. beki mstaarabu

Hii ni baada ya mechi wachezaji wakajiunga na mashabiki wao kucheza kiduku

MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA KIISLAMU CHINI YA ULINZI MKALI WA POLISI

Na Solomon Lekui


Waziri wa elimu Dk. SHUKURU KAWAMBWA akizungumza na wanafunzi wa kiislamu jijini Dar es salaam katika maeneo ya kidongo chekundu
Dk. SHUKURU akiondoka maeneo hayo chini ya ulinzi mkali wa polisi


wanafunzi na mabango mbali yenye jumbe mbalimbali






Wanafunzi wa kiislamu shule za sekondari za Dar es salaam wameandamana jana kama walivyoahidi siku chache zilizopita kwenye vyombo vya habari. Maandamano yao yaliishia viwanja vya kidongo chekundu na waziri wa elimu Dk.shukuru kawambwa alikuwepo kuongea nao.