Monday, June 11, 2012

Buriani Mzee Bob Makani,Daima tutakukumbuka mpiganaji

Na Solomon Ole Lekui


ALIYEKUWA Muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mohamed Bob Makani amefariki dunia, maafisa wa Chadema wamethibitisha.

Makani amefariki Dunia jioni ya leo jijini Dar kwenye hospital ya Aghakhan, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amethibitisha hilo kwa njia ya simu kutoka Kanda ya kusini walikokuwa wakifanya mikutano yao ya hadhara.

Mbowe amesema Marehemu Makani alikuwa akiugua kwa muda mrefu na kupelekwa hospitali mbalimbali kwa matibabu ikiwemo nje ya nchi.
Amesema mwili wa Marehemu umehamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa hifadhi. Msiba upo nyumbani kwake Mbezi Beach jirani na Rainbow.

 Watu wakiaga mwili wa marehemu Bob Makani
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiwa na viongozi wakuu wa Chadema, Freeman Mbowe (mwenyekiti) na Dk Willbroad Slaa (Katibu) kuuga mwili wa marehemu Bob Makani, leo Karimjee.


Ukalale mahali pema mzee Bob Makani

Thursday, June 7, 2012

Taswira Mbalimbali Za Muendelezo Wa Operesheni Okoa Kusini inayofanywa na CHADEMA

Na Solomon Ole Lekui

 Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wananchi Masasi mjini
Mbunge wa jimbo la Ubungo (CHADEMA) John Mnyika akipandisha bendera ya chama nje ya ofisi ya CHADEMA Kijiji cha Mkangaula
  Pichani ni Mwenyekiti Freeman Mbowe akikata utepe wa kufungua Ofisi ya CHADEMA Kijiji cha Mkangaula. Ilikuwa ni baada ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa kutoa hotuba ya ufunguzi na John Mnyika kupandisha bendera ya chama nje ya ofisi hiyo, ikiwa ni ishara ya kupiga hatua katika mapambano ya awamu ya pili.
 Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika akitoa 'somo' kwa wanakijiji wa vijiji vya Kata ya Lumesule. Mapema Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika alikaribishwa na kuzungumza na Katibu wa Tawi wa CUF, Bi. Zaituni. Wananchi walimwelewa vyema. Kadi zikauzwa vizuri. Akaacha uongozi wa muda wa tawi lenye wanachama wa 34. Katika Kijiji hicho cha Lumesule,
  Mwananchi mmoja kwa jina la Yasin Mohamed alihoji Ya Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika (Kulia)ilikuwaje CHADEMA wakaachia Dkt. Slaa ashindwe urais, wakati alichaguliwa kwa kura nyingi na wananchi na wao wanajua alishinda uchaguzi huo wa mwaka 2010.

 John Mnyika akiwa katika vijiji vya Kata za Makukwe na Mkwedu, wilayani Newala. Kwa George Mkuchika ambako alikutana na kiashiria cha wazi kuhusu udhaifu wa Waziri Mkuchika (Mbunge wa Newala) katika kusimamia majukumu yake, baada ya wananchi katika Kijiji cha Tengulengu, Kata ya Mkwedu kumlalamikia kuwa Diwani wa Kata hiyo, Juma Dadi hajawahi kufungua ofisi yake zaidi ya mwaka mmoja sasa. Pamoja na kuwasilisha malalamiko yao kwa barua Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala na kwa Mbunge wao, Mkuchika, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
 Unaweza kuona pia wanawake wakiitikia PEOPLES POWER, nao wakaipiga ya nguvu kweli kweli kuonesha umoja na mshikamano katika Falsafa ya Nguvu ya Umma ya CHADEMA, katika kudai uwajibikaji, kupigania haki, uhuru na mabadiliko ya kweli ya mfumo na utawala nchini.
 
 Sehemu ya Umati mkubwa wa wananchi kwenye mkutano huo
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa akizongwa na wananchi wa Kijiji cha Namahinga, Masasi aliokuwa akisalimiana nao.
 Opresheni Okoa Kusini katika picha, hapa ilikuwa Masasi Mjini. Waweza kuona katika baadhi ya picha watu walivyopanga mstari kupigania kadi.Picha na Habari na Kurugenzi ya Habari- CHADEMA

CHADEMA yawa gumzo Marekani, vua gamba vaa gwanda!!


Na Moi Dodo

Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Kalley Pandukizi akiwa na katibu wachama hicho,Ndugu Libe Mwang'ombe alipotoa kadi rasmi kwa Beautician maarufu na designer wa kiTanzan Linda Bezuidenhout (LB)

Katika miaka ya nyumba Linda aliwahi kusponsor matukio mbali mbali kwenye miaka ya 1990 wengi wao wakimjua kwa Linda Express Nchini Tanzania ambae ambaye hivisasa anajishughulisha na biashara ya nguo za kiume milanovita.com pamoja na zakike ambazo anadesign mwenyewe kwa brand name ya Linda kutoka Atlanta, Georgia Nchini Marekani.



Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi, pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe akimkabidhi rasmi mwanacham mkareketwa ambae ni mwana mitindo Linda Bezuidenhout (LB) kati ya uwanachama wa chama cha Demokrasia Chadema katika ofisi ya tawi la Tawi la Chama Washington DC.



Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Washington DC Mhe. Kalley pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe wakipata picha ya pamoja na Linda Bezuidenhout Atlanta, Georgia na wanachama wa tawi la chadema Washington DC



Viongozi wa tawi la chadema Washington DC wakipata Champagne


Linda Bezuidenhout (LB) furaha baada ya kuvua kamba kuvaa gwanda na kuchukua kadi kuwa mwanachama kamili wa
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Wednesday, May 30, 2012

Taswira Mbalimbali Za Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohd Aboud na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Saidi Mwema Walipotembelea Kanisa Lilochomwa Moto Huko Zanzibar

 Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud akielezea jambo kwa Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga wakwanza kulia kuhusiana na kuchomwa moto kwa Kanisa hilo liliopo Kariakoo Mjini Zanzibar katikati ni  Mkuu wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwemwa.
 Mku wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwema akitoa hotuba kwa Maaskofu na baadhi ya waumini wa Kikristo katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar lililochomwa moto,ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.kuliani kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Abdalla Mwinyi na kushoto yake ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Abdalla Mwinyi Khamis akitoa hotuba na kuonyesha Umoja na Mshikamano uliokuwepo kati ya Waislam na Wakristo kwa Picha ambayo imebuniwa na Mchoraji wa kingereza na kuwataka kuendelea na mshikamano wao ili kuzidi kuleta amani nchini.
 Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akielezea  kwa Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud na Viongozi wengine mbalimbali kile kilichotokea baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
 Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akibubujikwa na Machozi kwa kuguswa na hotuba iliokuwa ikitolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tukio hilo.
 Mkuu wa Dini ya Kiislam Afisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Noman Jongo akitoa hotuba ya Dini inavyoeleza kuhusiana na kudumisha Amani na Usalama katika nchi na kuondosha mifarakano na chuki na kuharibu mali.Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar ambalo limechomwa moto.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akimuonesha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud maeneo yalioathirika zaidi baada ya Kanisa hilo kuchomwa moto katika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.Picha na Yussuf Simai-Zanzibar

Friday, May 25, 2012

Taswira:John Mnyika(CHADEMA)Mbunge Halali Jimbo La Ubungo


 Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA), John Mnyika akiwa amenyanyuliwa juu na wafuasi wa chama hicho baada ya kushinda kesi.
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. John Mnyika akiwa amebebwa juu juu na Wanachana wa Chama hicho pamoja na washabiki wake nje ya Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam leo mara baada ya kushinda kesi yake iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na Ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
 Mbunge wa ubungo John Mnyika katikati akiingia Mahakamani jana
 Mh. Mnyika alipokuwa akiwasili Mahakamani jana asubuhi.
  Mnyika akipongezwa na Baadhi ya jamaa zake waliofika Mahakamani hapo.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akipeana mkono na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
  Baada ya kutolewa kwa hukumu na Jaji Upendo Msuya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wapenzi na mashabiki wa Chadema walilipuka kwa furaha.
 Baadhi ya wafuasi wa CCM wakiwa Mahakamani.
Baadhi ya Waandishi wa Habari, wa pili kulia ni Happiness Katabazi kutoka Tanzania Daima
Baadhi ya wafuasi wa Chadema wakiwa nje ya jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania jana asubuhi katika kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Hawa Ng'umbi.
 Askari Polisi wakihakikisha usalama upo wa kutosha katika njia walizokuwa wakipita wapenzi wa Chadema kusherehekea ushindi wa Mbunge wao

Monday, May 14, 2012

CCM watumia mapanga kuvuruga mkutano wa Peter Msigwa

Na solomon Ole lekui


Akiwahutubia wananchi kijiji cha nduli kilichopo manispaa ya iringa.



Sehemu ya umati wa wananchi.


Akimtambulisha mtu aliyekua mwenyekiti wa ccm katika eneo hilo alie jiungana chadema akiwa na wanachama wengine zaidi ya 100 wakimfuata.


wakati akimalizia mkutano, vijana wanao daiwa kuwa ni watoto wa diwani wa eneo lile walivamia mkutano nakuanzisha vurugu wakitaka kumvamia Mh. msigwa. nakusababisha vurugu iliyo peleke kukatwa mapanga kwa vijana wa wili wa chadema, mmoja kukatwa mkono na mwingine kujeruhiwa vibaya usoni. vijana hao waliokua wamekusudia kumdhuru mh. msigwa


kijana wa chadema alie katwa mkono na vijana wa ccm ambao wanasemekana kuwa ni watoto wa diwani ccm wa eneo hilo.


vijana hao walio leta vurugu katika mkutano kwea sasa wanashikiliwa na polisi.

kesho mh. Msigwa ana tarajia kuongea na vyombo vya habari kuhusu yalio tokea leo.