Sunday, July 22, 2012

Haya ndio mapokezi ya Mabingwa wa Kopa Cocacola {2012} Morogoro




Tatizo la Maji litaisha lini?



Na. Hatibu jumbe
Ni miaka hamsini sasa tangu Tanzania ijipatie uhuru wake toka kwa wakolon,kwa lengo la kujiendeshea maisha yao wenyewe.Katika kipindi chote hicho bado suala la upatikanaji wa maji safi na salama limekuwa likisuasua hasa kwa wakazi wa vijijini.
Suala la upatikanaji wa maji limekuwa ni tatizo sugu la licha ya kuwepo kwa sera na kaulimbiu mbalimbali zinazo tolewa kila mwaka zikiwa na dhumuni la kuboresha na kurekebisha upatikanaji wa maji mijini na vijijini.

Si ajabu kuona misururu ya ndoo kwenye mabomba au watu na mikokoten yao kueleke bombani katika miji kadhaa hapo Tanzania. Imesha wahi kuriportiwa kupitia vyombo kadhaa vya habari kuwa mikioa ya Morogoro, Dodoma, Singida na baadhi ya maeneo ya Dar es sallam kukabiliwa na adha ya maji katika misimu mbalimbali ya majira.
Mara nyingi wahanga wakubwa wa janga hili ni wanawake ambao huwajibika kutafuta maji toka pale yanapopatikana mpaka nyumbani, ambapo maranyingi huyatoa umbali mrefu. Hali hii inakwamisha juhudi nzima ya maendeleo kwani badala ya watu kujumuika katika shughuli nyingine za kimaendeleo wanaishia kupanga misururu na foleni katika mabomba ya maji na vyanzo mbalimbali vya maji.

Maadhimisho ya wiki ya maji mwaka huu kitaifa yamefanyika mkoani Iringa yakiwa na kaulimbiu inayosema “Maji kwa Usalama wa Chakula” 

Mipango ya utekelezaji ya Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira iliyozinduliwa na rais Jakaya Kiwete mwaka 2007, ililenga kuongeza upatikanaji wa huduma za majisafi na salama katika miji mikuu 19 ya mikoa (ukiacha Dar es Salaam na Pwani) kutoka asilimia 78 mwaka 2006 hadi asilimia 90 mwezi Desemba mwaka 2010. Hadi ilipofika Desemba 2011, hali ya upatikanaji wa huduma za maji safi na salama katika miji hiyo ilikuwa asilimia 88 ambapo lengo halikufanikiwa kwa asilimia 2

Katika maeneo ya vijijini, lengo lilikuwa kuongeza Desemba mwaka 2006 hadi asilimia 65 ifikapo mwezi Desemba 2010. Hadi Desemba 2011, upatikanaji wa huduma za maji vijijini ulikuwa katika wastani wa asilimia 58, ikiashiria kuhitajika kwa juhudi za ziada ili tuweze kufikia lengo. Juhudi hizo za ziada ni pamoja na zile zinazohitajika kutekelezwa ili kuboresha huduma za maji katika Jiji la Dar es Salaam, katika miji mikuu ya wilaya na miji midogo.

Licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali na mashirika binafsi katika kutatua tatizo hili la maji ni kama mradi wa visima vijijini, dhahir kuwa juhudi hizo zimegonga mwamba kwani wananchi waliowengi wanakabiliwa na tatizo hili.
Hakuna asiye tambua kuwa ukosefu wa maji  huweza kuhatarisha maisha ya binadadamu na hata kupelekea kifo kwani maradhi mbalimbali ya milipuko huibuka kama kipindupindu kutokakana na kunywa maji yasiyo safi na salama.

Kwa namna moja ama nyingine wananchi wanahusika moja kwa moja katika kufaya rasilimali ya maji kupotea kwa kulima kando kando ya vyanzo vya maji au kukata miti.
Wote tumeshaona kile kinacho tokea Somalia jinsi watu na mifugo inavyoteketea kwa ukosefu wa maji.  Takwimu zinasema kwamba kutakuwa na ukosekanaji wa maji ifikapo mwaka 2025 endapo vyanzo vya maji vilivyopo sasa havitotunzwa.

Miradi mbalimbali imekuwa ikianzishwa kama vile za kilimo cha umwagiliaji, ufugaji huku sekta hizi zote zikiwa na vikwazo vikubwa vya ukosekanaji wa maji ya kutosha.
Hatunabudi wananchi tuunge mkono juhudi zinazofanywa na serikali juu ya upatikanaji wa maji safi na salama ikiwemo kutunza vyanzo vya maji na kuwafichua waharibifu wa vyanzo hivyo, pia tuache tabia ya kupasua mabomba ya maji.

Vilevile kwa upande wa serikali ihakikishe miradi anzilishwi ya maji ipewe watendaji waaminifu kwani baadhi ya watendaji kwenye kamati hizo hufanya ubadhirifu wa hela za miradi bila kujali wananchi wanaathirika kwa kiwango gani

Saturday, June 30, 2012

DOKTA ASHA-ROSE MIGIRO AWA MJUMBE WA MASUALA YA UKIMWI BARANI AFRIKA.


       Na Consolata Haule
         
      Aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa  Afrika dokta Asha-Rose Migiro         ameteuliwa    na katibu mkuu wa umoja wa mataifa   mheshimiwa Ban Ki Moon kuwa mjumbe wake maalum wa masuala ya Ukimwi barani afrika baada ya kumaliza mda wake.
    
       Alitangaza uteuzi huo katika hafla ya maaulum  aliyoondaa kwa ajili ya ya kumuuga Naibu Katibu Mkuu wake  ambaye amemaliza muda  wa uongozi  wake kwa muda wa miaka mitano na nusu katika nafasi ya  Unaibu Katibu  Mkuu.
  
        Hafla hiyo ilifanyika  katika wiwanja vya Umoja wa Mataifa na kuweza kuhudhuria na  wageni waalikwa wengi  mabalimbali na mashuhuru duniani wakiwemo mabalozi wan chi mbalimbali, wakuu wa mashirika  ya Umoja wa Mataifa. 
     
   Ametangaza rasmi kwamba amemteua dkt.  Asha- Rose Migiro kuwa  mjumbe wake maalum katika masuala ya ukimwi na ugonjwa wa Ukimwi Barani  Afrika. aliongeza kwa kusema  Ban Ki Moon. aliendelea kwa  kueleza kwamba ingawa Migiro alikuwa naibu katibu mkuu wake, lakini amekuwa mwalimu wake, na amejifunza mengi toka kwake na daima ataendelea kuuenzi mchango wake mkubwa aliofanya pindi alipokuwa kazini.

   “ Kama ni kuvaa viatu vyake, naweza kusema ningechekesha sana,  kwa ufupi siwezi kuvaa viatu vya Migiro, amekuwa msaada mkubwa sana kwangu, ameniwakilisha vema kila mahali nilipomtuma hata katika mazingira magumu na ya hatari,  kote ameniweza kuniwakalisha vema kiukweli. kama  mwalimu wangu, na kama profesa wangu anastahili alama ya juu sana” alisema  Ban Ki Moon na kushangiliwa.

   Alizidi kumuelezea  Migiro kama kiongozi si tu mwadilifu, lakini mwanadiplomasia  aliyebobea, aliyefanya kazi kubwa,ngumu na nzito kwa moyo mkunjufu, uhodari , umakini, na uadilifu wa hali ya juu sana.

    “ Siyo rahisi kuelezea yale aliyoyafanya nyuma ya pazia, namna gani alivyochapa kazi kwa nguvu, yapo mengi makubwa ambayo Migiro ameyafanya na  kuyakamilisha kwa uadilifu wa hali ya juu. Migiro ni mwanadiplomasia aliyebobea lakini ni mtu wa vitendo, vitendo ambavyo lazima utaona matunda yake” akabainisha Ban Ki Moon.

    Na kuongeza “  Migiro amefanya kazi na viongozi wagumu,  akiwemo aliyekuwa  Rais wa Libya Muammar  Quadaff aliyethubutu hata kumrushia katiba ya Umoja wa Mataifa, kiukweli ameweza kuzikuna nyonyo za watu wengi wakiwamo watu wanyonge na wenye matatizo mbalimbali duniani.Vilevile ameweza  kuondokana migogoro inayoendelea duniani. hivyo lakini Umoja wa  Mataifa hautasahau mchango wake.

      Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  alliweza kuitumia fursa hiyo  kwa kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini ya raisi wake Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumruhusu Migiro kwenda kuitumikia jumuia ya kimataifa.

   “ Ninapenda  kutoa shukrani zangu za pekee kwa  jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa kumtoa Migiro katika utumishi wake wa Umma kuja kunisaidia , kwa serikali ya Tanzania na  watanzania nasema asanteni sana” alisema Ban Ki Moon..

     Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu dkt. Asha-Rose Migiro amesema anaupokea kwa mikono miwili uteuzi wa kuwa mjumbe maalum wa Katibu Mkuu katika masuala ya Ukimwi barani Afrika.

      Alizidi kusema   masuala ya  ukimwi na ugonjwa wa ukimwi, ni eneo ambalo limo ndani ya moyo wake na kwamba anashukuru kuona kwamba Katibu Mkuu anamuamini anaweza kumsaidia. Aliaahidi  atalitekeleza  jukumu  hilo kwa heshima  kubwa aliyopewa na Katibu Mkuu.
       Pia alimshukuru Ban Ki Moon kwa kumuamini kwamba anaweza kumsaidia kama naibu Katibu Mkuu, na akamshukuru pia kwa ushirikiano mkubwa na uhusiano mkubwa uliojengeka kati yake na Ban Ki Moon lakini pia kati yake na wasaidizi wake.  Ushirikiano ambao alisema ulichangia utendaji mzuri wa kazi na kufanikisha dira na matarajio ya Katibu Mkuu.

      “Katibu Mkuu amenipa heshima ya kihistoria, heshima ya kuwa msadizi wake,  ni heshima kubwa kwangu na kwa yeyote atakayekuja kuandika historia yangu, kwa namna yoyote ile hawezi kukwepa  kumtaja  Ban Ki Moon, naomba nikushukuru sana kwa heshima hii kubwa uliyonipa” alisema Migiro.

      Katika hafla hiyo pia ilihudhuriwa  na familia ya Naibu Katibu Mkuu ikijumuisha  mume wake, Profesa  Cleophas Migiro,  mdogo wa  Naibu Katibu Mkuu, Bi. Amina  Mtengeti na mtoto wao wa  mwisho wa Migiro Chansa Jasmin.

    Naibu Katibu Migiro anakuwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo na mwanamke mwafrika wa kwanza. Lakini pia ni naibu katibu mkuu ambaye amehudumu katika wadhifa huo kwa miaka mitano na nusu.
Dokta Asha-Rose Migiro akizungumza na kutoa shukrani katika hafla hiyo.

         Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa anazungumza na wageni waalikwa hawapo pichani,kulia  ni Dkt. Migiro na katikati ni Mkurugenzi wa ofisi ya Naibu Katibu Mkuu, Bwana  Anyanga

Thursday, June 28, 2012

COCA COLA WAANDAA TUZO ZA WAANDISHI BORA WA MICHEZO WA COPA COCA COLA

    Na Consolata haule
              
     Coca-Cola Tanzania imetangaza kuanzisha tuzo kwa waandishi bora wa michuano ya soka ya vijana ya Copa Coca-Cola kwa nia ya kuwazawadia wanahabari wanaofanya kazi nzuri katika michezo,hivyo kuwa chachu ya mashindano ya Copa-Cola yenye lengo la kujenga
msingi wa maendeleo ya soka nchini Tanzania.
 
             Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa Coca Tanzania Salome Mabirizi alisema kuwa Coca-cola inatambua mchango mkubwa uliofanywa na waadishi wa habari kwa miaka mitano iliyopita katika kuwahamasisha kushiriki mashindano haya. Kuanzishwa kwa tuzo hizi ni njia moja wapo ya kuwashukuru waandishi wa habari kwa kazi nzuri ya kutangaza Coca-Cola.
 
           Alizitaja tuzo hizo kuwa ni mwandishi bora wa magazeti, mwandishi bora wa luninga, mwanahabari bora wa radio, mpiga picha bora (magazeti) na blogs bora, ambapo kila mshindi ataweza kuzawadiwa  thamani ya milioni 2 taslimu za kitanzania.

               Mchakato wa kuwapata washindi utafanywa kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na Coca-Cola na tayari zoezi hilo limeshaanza tangu Jumapili juni 24 wakati fainali za Copa Coca-Cola Taifa zilipozinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam na  Fainali hizo zimepangwa kumalizika  Julai 15.
 
         Katibu Mkuu Msaidizi wa TASWA, George John aliwaambia waandishi wa habari kuwa kamati ya tuzo za Copa Coca-Cola itafanya kazi kwa kuzingatia vigezo ili kuweza kumpata mshindi anayestahili katika kila kundi lililotaja hapo juu.Pia amevitaja baadhi ya vigezo hivyo kuwa ni pamoja na stori au makala zinazohamasisha na kuwatia moyo vijana kuweza kuonyesha na kuendeleza vipaji vyao.
 
            Johan ameipongeza kampuni ya Coca-Cola kwa kushirikiana na Shirika la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuendesha mashindano hyo kwa nchi nzima kwa lengo la kuibua vipaji vya wanasoka chipukizi nchini Tanzania.
 
        Kiukweli Copa Caca_Cola imesaidia kubadili sura ya mpira wa miguu nchini Tanzania kwa kuwa chanzo cha kutegemewana wachezaji wenye vipaji wa kila timu za ligi kuu na timu za Taifa.  
NI mashindano pekee nchini ambayo huchezwa nchi nzima kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa yakishirikisha maelefu ya vijana kila mwaka ili kuwaendeleza vijana zaidi. 
 
        Coca-Cola imekuwa ikipeleka wachezaji bora wa Copa Coca-Cola kwenye kambi za kimataifa za mafunzo ya soka nchi za nje. Mnamo Mwaka 2007 na 2008 wachezaji bora wa Copa Coca-Cola walikwenda nchini Brazil na kuanzia 2008 hadi mwaka jana walipelekwa Afrika Kusini.
 
    Coca-Cola ni kampuni yenye historia ndefu ya kusaidia michezo ilianza kudhamini michezo ya olimpiki tangu 1928 na mpira wa miguu tangu 1930.  Kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikidhamini Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) tangu 1974 na kuwa mdhamini rasmi wa FIFA tangu 1978 hadi sasa.
 
 
 
             Mkurugenzi mahusiano wa Coca Cola Kwanza( wa katikati )Bw. Evans Mlelwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za Coca Cola juu ya Tuzo kwa waandishi wa habari COPA COCA COLA,wa  kwanza kulia ni Katibu msaidizi  wa Taswa Bw. George John,kwa upande wa kushoto ni  Meneja Masoko wa Coca Cola Tanzania Bi.Salome Mabirizi.

HALI YA DK. ULIMBOKA ILIVYO SASA.



            Kama tunavyomwona Dk Ulimboka akiwa katika hali mbaya na huku akiwa ametundikiwa mashine maalum katika chumba cha wagonjwa wa mahututi  katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili- Dar- es -salaam.

Na Consolata Haule

MADAKTARI WAPATAO 72 WASIMAMISHWA KAZI MKOANI MBEYA.

  
Na  Consolata Haule

                
            Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewafukuza madaktari wapatao 72 kwa   kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume cha makubaliano ya mkataba wao wa kazini.
  
          Inasemekana  kuwa madaktari hao ambao 54 ni wale wa mafunzo ambao waliingia mkataba wa miaka miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari 18 ni wale walioajiriwa na Wizara ya afya. 
          
         Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti kazini kwa siku tano ni ukiukwaji wa kanuni za utumisha wa umma hivyo kupitia kanuni hiyo ya utumishi wa umma madaktari hao wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi za kinidhamu alizidi kunena.
        
        Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Bodi, imeelezwa kuwa siku ya tarehe 23/6/2012 wafanyakazi 15 waliokuwa zamu hawakufika kazini na tarehe 24/6/2012 wafanyakazi 19 hawakufika kazini. 
        
       Alizidi kusema kuwa kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo imethibitika kuwa 72 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012.Na mnamo tarehe 25/6/2012 bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura ili kujadili hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa uamuzi juu ya jambo ilo.
        
       Aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na madaktari ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili namna ya kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao waligoma.

      Baada ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali iliwaandikia barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali na pia kukiuka kanuni za kudumu za utumishi wa umma nalo walilikaidi
      Alizidi kuongeza kwamba iwapo madaktari ambao hawakuripoti au kueleza sababu za kuridhisha ifikapo mpaka  tarehe 28/6/2012na kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma, madaktari hao watasimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
      
      Vilevile  alisema kuwa kwa ujumla madaktari hao waligomea barua zote mbili yaani ya kuitwa kwenye kikao pamoja na ile ya kuwataka kujieleza hivyo Bodi imechukua hatua za kisheria za kuwafukuza kazi.
    
      Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa bodi, alisema kuwa tayari hospitali ya Rufaa kwa ushirikiano wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, madaktari watano wamepatikana ili kusaidia huduma kwa hospitali hiyo.





             
                       Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kufukuzwa kazi kwa madaktari hao wapatao 72.

Monday, June 25, 2012

Na Hija MkalI

KESI YA LULU YAHAIRISHWA HADI JULAI 9 MWAKA HUU.


Msanii wa Film Elizabeth Michael maarufu kama Lulu,akisindikzwa na askari wa magereza kwenda kupakia kwenye basi la magereza,kurudishwa rumande hadi kesi hiyo otakapotajwa tena Juali 9.