Sunday, January 22, 2012

DK SLAA ANA KWA ANA NA RAIS KIKWETE IKULU.


Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa, Ikulu Dar es Salaam jana usiku katika muendelezo wa mazungumzo ya mchakato wa Katiba mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe na katikati ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Said Alfi. Picha na IKULU


RAIS Jakaya Kikwete amekutana na uongozi wa Chadema Ikulu Jijini Dar es Salaam, akiwemo Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa, kuzungumzia mchakato wa Katiba Mpya.Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili, mkutano huo ulifanyika jana kuanzia saa 10:30 jioni na kuendelea hadi usiku, lakini walifanya mapumziko mafupi saa tatu usiku.


Ujumbe wa Chadema uliokuwa wa watu wanane, ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe. Wengine waliofuatana naye pamoja na Dk Slaa ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, John Mnyika, Said Arfi, John Mrema, Profesa Mwesiga Baregu na Profesa Abdallah Safari. Hadi tunakwenda mitamboni kikao hicho kilikuwa kinaendelea.


Hii ni mara ya kwanza kwa Dk Slaa kukutana na Rais Kikwete tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2010, ambao Dk Slaa alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34 akiwa nyuma ya Rais Kikwete aliyepata kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17, Dk Slaa hakuwahi kukutana na mkuu huyo wa nchi ana kwa ana.
               
POSTED BY SIXTUS BAHATI.



No comments:

Post a Comment