Thursday, November 10, 2011

MUSA MAHUNDI KOCHA MPYA WA MPIRA WA MIGUU TUMAINI IRINGA

 By Hija Mkali

Kocha wa zamani wa klabu ya Polisi Iringa,Lipuli pamoja na timu ya Mkoa wa Iringa (Mkwawa Horeos),Musa Mahundi,amewasili jana katika kiwanja cha mpira wa miguu cha chuo kikuu cha Tumaini Iringa.

Mahundi,ameteuliwa na chuo kwa ajili ya kuisaidia timu katika mashindano ya vyuo vikuu nchini (Shimivuta),ambayo yanatarajiwa kuanza mnamo terehe 26 mwezi huu katika kiwanja cha Mkwakwani jijini Tanga.

Aidha,mahundi,''aliomba ushirikiano baina yake na wachezaji ili kudumisha nidhamu,uadilifu ndani na na nje ya uwanja''.

Mahundi,''alianza kazi jana na kuangalia wachezaji atakao wafaa ili kwenda nao Tanga na kuleta ushindani mkubwa na kuweza kuleta heshima chuo (Tumaini Iringa)''.

Wakati huohuo,mlezi wa wanafunzi,mchungaji Oswald Ndelwa,aliwaomba wachezaji kumpa ushirikiano wa kutosha kocha (Mahundi),ili kukiletea heshima chuo chetu.

Kwa upande wake nahodha timu hiyo,George Kanji,aliwataka wachezaji wenzake kuleta mwamko baina yao.

Sanjari na kusema hivyo,ili soka la Tumaini,liendelee kuwepo na kukuwa hapana budi kuwepo kwa nidhamu,uadilifu na heshima baina yetu.

Programu ya mwalimu ni mpango ni muda mfupi wenye lengo la kuwajenga wachezaji kisaikolojia kwenye soka la ushindani,pia ani fursa ya kuona vipaji vipya vya wachezaji chipukizi na kutumia nafasi hiyo kuendeleza soka kwa faida ya badae.

No comments:

Post a Comment