Wednesday, November 30, 2011

Tusiendekeze fitina katika kuteua wachezaji wa timu ya chuo.


Ninachokiwaza.

Na Hija Mkali
 
"Panapo na riziki hapakosi fitina''huu ni msemo wa Kiswahili wenye maana ya kuwa popote panapokuwa na neema panakuwa na misuguano ya kimawazo ya hapa na pale, nimeanza kwa msemo kwa maana hii.

Katika uteuzi unaofanywa mara nyingi katika timu zetu za vyuo na hata pengine katika nchi panakuwa na migongano ama misuguano kutokana na viongozi kuchagua wachezaji wasiokuwa na uwezo/marafiki zao ili tu kupata chochote kitu toa  kwao..

Mathalani katika timu ya Chuo ya mpira wa miguu ya Tumaini,kumejaa urasimu mkubwa unaotokana  na urafiki na uzandiki uliojaa kwa viongozi,kuna wachezaji wameachwa na wana uwezo mkubwa wa kusakata"kabumbu" ila kutokana kutokuwa karibu na viongozi au ugeni wao katika timu ya Chuo ndio maana wameachwa au kusahaulikia.

Ninachofikiria kwamba tusije tukawa kichwa cha mwendawazimu huko wanakokwenda katika mashindano ya Vyuo Vikuu nchini(Shimivuta) yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni Mkoani Tanga.

Kwa mtazamo wangu kuna timu ambazo zimejitayarisha vizuri kwa ajili ya kubeba vikombe na medali,kuna baaadhi vyuo vikosi vyao vinaundwa na wachezaji wanaochezea ligi kuu ya Tanzania Bara na madaraja mengine na sitaki kusema tutafanya vibaya ila tusije tukawa wasindikizaji.

Kutokana na ili swala tunaomba viongozi timu ya chuo ya Tumaini ya mpira wa miguu waliangalie kwa jicho la tatu ili siku moja tuwe mfano wa kuigwa katika tasnia ya michezo ya vyuo vikuu nchini.

Kila la kheri timu ya chuo cha Tumaini Iringa katika michezo yote mtakayo tuwakilisha katika mashindano hayo. Ni imani  yangu mtarudi na vikombe na baadhi ya medali toka mkoani humo. .

No comments:

Post a Comment