Na John Alex.
Malalamiko yanayoendelea kutolewa na wanafunzi wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini ni dalili sio tu ya wasomi hao kutokuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na serikali katika kutatua changamoto zinazowakabili lakini pia kushindwa vikali kwa serikali iliyoko madarakani katika utekelezaji wa sera zake kuhusu elimu ya juu nchini.
Wote mtakubaliana na mimi kuwa wasomi wa vyuo vikuu nchini ni hazina kubwa sana kwa taifa la Tanzania kwani hao ndio chimbuko la mawazo mapya na uelewa na pia ni chazo kikubwa sana cha maendeleo ya taifa. letu kwani taifa bila wasomi ni sawa na Gari kubwa la mkaa litembealo njiani usiku bila taa wakati wowote laweza gonga mti au mwamba na kupinduka..
Matatizo yanayowakabili wanafunzi wasomi wa vyuo vikuu nchini ni mengi lakini leo nataka nizungumzie moja tu ambalo limekuwa changamoto kubwa sana kwa wasomi hawa wa vyuo vikuu na bado litaendelea kuwa changamoto yenye kuleta madhara makubwa endapo serikali na mamlaka husika hazitawajibika ipasavyo kutafuta ufumbuzi na kulitatua kabisa tatizo hilo.
Swala la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini limezua mjadala mzito sana kwa wanafunzi kwani wasomi hao wamekuwa wakiiomba serikali iongeze fedha za mikopo hususan fedha za kujkiimu wawapo vyuoni na pia ada ikibidi..Kilio hiki cha wanachuo ni cha muda mrefu sana. na wengi wamepoteza masomo kutokana na kushindwa kujikimu wenyewe kutokana na ugumu wa maisha ambao kimsingi husababishwa na kupanda kwa gharama za maisha .Bei ya bidhaa nchini inapanda kila kukicha na hivyo hata taasisi binafsi za elimu zote pia inawalazimu kupandisha gharama za utoaji huduma.
Baada ya kilio cha muda mrefu cha wasomi hawa kilichoambatana na maandamano na migomo kila kukicha serikali ikaanza walau kulifikiria na kuliangalia upya swala la mikopo na hatimaye kukiri kuwa ni kweli ghrama za maidha ya sasa si sawa na kiwango cha fedha za kujikimu walichokuwa wanatoa hadi hivi karibuni..Fedha ya kujikimu ya mwanafunzi mmoja kwa siku ilikuwa ni shilingi za kitanzania elfu tano tu.Hivyo serikali kwa kuliona hilo,ikaamua kupandisha kiasi cha fedha hizo kutoka shilingi elfu tano hadi elfu saba na mia tano kwa siku ambapo imeongezeka shilingi elfu mbili na mia tano tu ambayo imeanza kulipwa rasmi mwaka huu wa masomo.
Hata hivyo ongezelo la kutoka shilingi elfu tano kwa siku hadi elfu saba na mia tano halikuwa makubaliano kati ya wanafunzi wa vyuo vikuu kote nchini na serikali bali wasomi hao waliiomba serikali kutokana na kupanda kwa gharama za maisha ongezeko la kutoka elfu tano hadi elfu kumi kwa siku.Hapa tunaona kuwa serikali haijatekeleza wala haijatoa suluhu bali imefanya kwa sehemu tu kitu ambacho hakijawaridhisha wasomi hawa hata kidogo na ndio maana hata makala za kuipongeza serikali kwa utekelezaji huo hakuna!
Pamoja na kukubaliana na hali halisi ili kutopoteza wakati,wanafunzi wasomi hawa wote wameamua kujikalia kimya huku wakijiliwaza na kauli za wahenga kama vile, mvumiivu hula mbivu,na kwa ahadi za seikali za tutafanya, basi wasomi hawa pia wanarejea kwenye kauli za wahenga kuwa subira yavuta kheri.
Sasa tayari wanafunzi hawa wako vyuoni, lakini badala ya kupungua maumivu ndio kwanza yameongezeka.Mamlaka iliyokabidhiwa dhamana ya kushughulikia pesa za wanafunzi ziwafikie kwa wakati yani Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu,(HSLB) inaonyesha kushindwa kabisa kutekeleza jukumu lake,hali inayofunua hisia mpya kuwa kuna urasimu mkubwa ndani ya chombo hicho cha serikali ambacho chenyewe pia kinatupa lawama kwa serikali kwamba hatujapokea pesa kutoka serikalini.
Kutokana na kutokuwajibika kwa bodi ya mikopo na urasimu uliopo pamoja na rushwa iliyokithiri, serikali kutolichukulia uzito swala hili,madhara makubwa yanaendelea kutokea, ambapo mwaka huu takribani wanafunzi wapatao elfu kumi na nne wamekosa mkopo je watakwenda wapi wale watoto wa wakulima?
Kumeundwa bodi ndogo za mikopo vyuoni na serikali imetoa tamko kuwa fedha za mikopo zitapelekwa vyuoni jambo ambalo ni kukiuka mkataba kati ya bodi ya mikopo na wanafunzi wanaoendelea na masomo kwa mwaka wa pili na kuendelea kwa sababu haukuwa hivyo.Fedha zilitakiwa zipelekwe moja kwa moja kwenye akaunti za wanafunzi wenyewe ili kuondoa walau kwa sehemu tatizo la ucheleweshaji wa fedha za kujikimu na ada kwa wanachuo hawa kwani baadhi ya vyuo wamekuwa wakichelewesha sana fedha za kujikimu kwa wanafunzi.
Kumeibuka hisia miongoni mwa wanafunzi wa baadhi ya vyuo hapa nchini kuwa kuna vyuo vikuu vinavyopewa kipaumbele aidha kwa kuviogopa au kwa namna yeyote ile ya kiupendeleo.Wasomi hawa wa wa vyuo baadhi wameilaumu mamlaka husika kwa kuchelewesha fedha za vyuo vyao huku huku wakihoji kwanini vyuo vingine vipewe fedha kwa wakati na vingine visipewe kwa wakati?
Ni dhahiri kuwa serikali kutokana na kutojali na kutokulipa kipaumbele swala hili inashusha kiwango cha elimu nchini kwani migomo itaendelea kila kukicha na ndio maana hatukosei kabisa kusema kuwa serikali itegemee migomo zaidi kwani tatizo linazidi kuwa kubwa a badala ya kupungua.
Serikali haina budi kulitizama upya swala hili na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu kama inavyohangaika na kuimarisha miundombinu ya barabara kuu nchini ambapo kwa kweli inafanya vizuri sana huko.
Aidha serikali haina budi kuiwajibisha menejimenti ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini na kuhakikisha kuwa inaunda menejimenti madhubuti ambayo itafasnya kazi kwa umakini mkubwa na kwa haki huku mamlaka iliyokabidhiwa dhamana ya kuzuia na kupambana na rushwa ikiwa karibu kabisa na hivyo kuzuia urasimu na rushwa ambayo kimsingi ndio chanzo cha matatizo.
John Alex Mganga-0658385435
E.mail-Johnmganga@yahoo.com.
No comments:
Post a Comment