Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia mikutano ya kumnadi mgombea wake Joshua Nassari juzi na jana, ametoa mwaliko kwa wanachama na wafuasi wote wa chama hicho kwamba wafike kwenye mkesha wa kusubiri matokeo ya uchaguzi huo eneo la Leganga, jirani na Halmashauri ya Meru.

Mbowe alisema mara baada ya kubandikwa kwa matokeo katika vituo vyao, wapiga kura kwa pamoja wanapaswa kuelekea katika eneo la Leganga kusubiri matokeo ya uchaguzi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mulala, Kata ya Songoro nyumbani kwa mgombea wa chama hicho, Nassari, Mbowe alisema: “Naomba mara baada yakupiga kura, utakaa mita 103 kutoka kwenye kituo, hadi matokeo ya kituo chako yatakapobandikwa, chukua kanga, baiskeli, punda, gari au usafiri wowote tukutane Usa River ambapo tutafanya mkesha wa kusubiri matokeo.”

Alisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba kuna shinikizo la kumtaka Msimamizi ya Uchaguzi, Kagenzi atangaze matokeo tofauti hata kama Chadema watakuwa wameshinda.

“Ndugu zangu msigope kitu, tutakwenda kulala wote Usa River kusubiri matokeo yetu na kama wakitubia haki ya Mungu safari hii hatutakubali,” alisema Mbowe. Mbowe aliwataka polisi siku ya uchaguzi kuwaacha Chadema na CCM wachuane wenyewe kwani kazi yao ni kulinda amani na siyo kuilinda CCM.

Mapema Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema aliwataka wakazi wa jimbo hilo, wasiwena hofu ya wingi wa polisi katika maeneo yao akisema haijawahi kutokea hata siku moja bunduki ikazidi nguvu ya umma.

“Makamanda jitokezi kupiga kura kuanzia saa 12:00 jioni mkimaliza msubiri matokeo na baada ya hapo tukutane Usa River na hapo kutakuwa na makada wenzenu kusubiri matokeo.”

Katika mkutano huo, Viongozi wawili wa CCM, akiwemo Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa Tawi la Mulala, Eribariki Manjeka alirudisha kadi ya CCM na kujiunga na Chadema pamoja na William Nassari ambaye aliwahi kuwa Katibu Mwenezi na Itikadiwa CCM katika kata hiyo.

Kwa watu wenye akili za kawaida wanajua umuhimu wa kumchagua Nassari kuliko mtu wanaejua kuwa hatofanya kitu daima. Kama babake alishindwa akiwa Naibu waziri wa fedha, je wewe atawezaje
Click image for larger version. 

Name: bbb.jpg 
Views: 0 
Size: 92.2 KB 
ID: 50276
Mgombea wa CHADEMA akiomba ridhaa ya kuongoza wana wa Arumeru jana

Click image for larger version. 

Name: aaaa.jpg 
Views: 0 
Size: 533.4 KB 
ID: 50275Click image for larger version. 

Name: ccc.jpg 
Views: 0 
Size: 582.5 KB 
ID: 50277Click image for larger version. 

Name: ddd.jpg 
Views: 0 
Size: 415.6 KB 
ID: 50279