Ukilitazama swala la sakata la mgomo wa madaktari juu juu unaweza kuwalaumu na kuwaita watu wasio na huruma na hawawatendei haki wagonjwa,wauaji,wasaliti,wamek iuka kiapo cha udaktari n.k. Kitu ambacho serikali JK na utawala kwa ujumla katika propaganda na porojo zao wanataka tuamini hivyo.

Ukilitazama kwa ndani,wakualaumiwa na kubeba lawama zote ni Mh.Rais JK,serikali na chama Tawala CCM kwa sababu zifuatazo JK katika uteuzi wa mawaziri na nafasi mbalimbali katika serikali na taasisi mbali mbali hazingatii uwezo,uzoefu na sifa za mchaguliwa bali uswaiba na masilahi katika makundi ndani ya chama tawala.

Hali ambayo inampa hali ngumu ya kutoa uamuzi wa kuwawajibisha wanapofanya ndivyo sivyo.Tatizo lingine kwa vile serikali na utawala hauna dhana ya kuwatumikia wananchi hivyo kauli nyini na ahadi wanazozitoa zinatoka katika ulimi na kubaki katika makaratasi bila kufanyiwa utekelezaji kwa maana ya kua za kisanii na porojo ili muda upite. Hakuna anaewajibika kwa kauli au ahadi serikali au JK inazozitoa kwa hali hii kutegemea ufanisi ni ndoto ya mwendawazimu.

Mambo mengi yametokea(ufisadi,rushwa,uzembe n.k) katika serikali na viongozi katika serikali na taasisi za serikali hakuna anayejiuzulu au kuwajibishwa tume baada ya tume imekwisha.Hata huko katika CCM viongozi wanaopatikana huko ni kwa njia ya rushwa na ufisadi ambapo hao ndio viongozi baadae katika serikali.

NENO KUJIUZULU KUWAJIBIKA KATIKA UTAWALA HUU HALIMO KATIKA MSAMIATI WAO.NJIA PEKEE YA KUWALAZIMISHA WAWAJIBIKE NI MIGOMO NA MANDAMANO HIVYO MGOMO WA MADAKTARI UMEONYESHA NJIA JINSI YA KUIBANA SERIKALI ITIMIZE AHADI ZAKE NA SIO POROJO.MUNGU IBARIKI TANZANIA.