Monday, March 12, 2012

Uzinduzi wa kampeni za CCM arumeru

Na solomon ole lekui

Baada ya chama cha demokrasia na maendeleo kuzindua kampeni zake huko arumeru ya mashariki siku chache ilizopita, chama cha mapinduzi nacho kimezindua kampeni zake leo hii. Vyama hivyo viwili vimezindua kampeni hizo ikiwa ni nafasi ya kipekee kwao kuwanadi wagombea wa kiti cha ubunge kupitia vyama vyao baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo solomon sumari kuaga dunia miezi michache iliyopita.

wakiongeaa kwa mbwembwe na bashasha, wabunge na viongozi wa CCM wameapa kushinda katika uchaguzi huo kwani CCM ni chama kilichokomaa na chenye sera nzuri.

Mabasi mengi yalionekana yakiingia kutoka sehemu mbalimbali kama engereyan,ngabobok na maeneo ya mbali ya jimbo hilo kuja kushuhudia uzinduzi huo. Aliyeandalia kuzindua kameni hizo ni rais wa awamu ya tatu mh. mkapa a.k.a Mr. clean


Mh. john komba

Basi la kampuni ya URIO safaris lililokuwa likiwatoa watu kutoka maeneo mbalimbali ya Arumeru kuja kushuhudia uzinduzi wa kampeni za CCM



wapenzi na wakereketwa wa CCM wakisubiri kwa hamu uzinduzi wa kampeni za chama chao



HATA WACHEZA TAARABU WALIKUWEPO



Picha zote kwa hisani ya http://www.mjengwablog.com/

No comments:

Post a Comment