Wednesday, December 7, 2011




.
 Mojawapo ya nyumba zilizokumbwa na maji Tumaini.


Na John Alex


Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo tofauti mkoani Iringa zimepelekea baadhi ya  njia kadhaa za  maeneo tofauti ya manispaa ya Iringa  kupitika kwa shida kutokana na  kufurika kwa mifereji na vijito vya maji hali inayosababisha  miundombinu  ya barabara na madaraja kupoteza ubora wake na  kuanza kuharibika.

Hali hii imrjitokeza katika maeneo kadhaa yamanispaa ya Iringa ambapo  baadhi ya maeneo hususan maeneo ya Semtema , Kihesa ,na  maeneo ya chuo kikuu cha Tumaini  njia zake  kufurika maji wakati wa mvua  hali inayopelekea wakazi wa maeneo hayo kupita kwa shida  kwenye madaraja ambayo wakati wa mvua yalifurika  maji.

Mvua zilizonyesha  siku ya jumaatano  zilifurisha  mifereji na  mito  katika maeneo hayo hali iliyosababisha usumbufu mkubwa sana kwa wakazi wa  maeneo hayo kupita kwa shida kwenye madaraja  ambayo yalijaa maji na kufanya  miundombinu  kuwa katika hatari ya kuharibika

Aidha mvua hizo zimehatarisha  baadhi ya nyumba zilizojengwa pembezoni mwa  mito na mifereji kwani  maji yalikaribia  karibu  na kuta za nyumba zilizoko kwenye maeneo ya  pembezoni mwa  mifereji hiyo.
Wakazi wa Semtema  wamesema kuwa mvua hizo  zilizonza kunyesh a hivi kariibuni  endapo zitaendelea kunyesha  zitaharibu miundombinu  ya barabara na madaraja kwani  hayakujengwa kwa  kiwango kinachotakiwa kuhimili mafuriko na mvua zilizokithiri.

Hata hivyo hali hiyo imejitokeza pia katika maeneo ya Zahanati  maeneo ya Mwangingo ambapo baadhi ya nyumba ziliingia maji na kusababisha wasiwasi mkubwa kwa wakazi wenye nyumba zao maeneo pembezoni mwa mto   kuhofia kukosa makazi  baada ya kushuhudia  maji yakiingia hadi ndani.

Wakazi wa maeneo hayo wamesema kuwa  endapo mvua hizo zitaendelea kunyesha zitaleta maafa makubwa ikiwa ni  pamoja na kupoteza maakazi  kwa  wananchi waliojenga nyumba zao pembezoni mwa  mito.

Hata hivyo baadhi  ya wakazi wa manispaa ya Iringa wameliambia kwanza jamii kuwa  mvua zinazoendelea kunnyesha zitapnguza ukame na  hivyo kufanya shughui za kilimo kuendelea vizuri lakini endapo zitaitiliza zinaweza ziksababisha hasara kwa mazao.

Mvua hizo zimesababisha uharibifu mkubwawa bostani za mbogamboga hususan kwa wakazi wa Tumaini ambao wamekuwa wakijihusisha na kilimo cha bostani za mbogamboga pembezoni mwa mto .

No comments:

Post a Comment