Sunday, May 6, 2012

CHUO KIKUU CHA TUMAINI CHAIBUKA WASHINDI DHIDI YA CHUO KIKUU CHA MZUMBE (MBEYA)

            

          Na Consolata Haule.
         
     Chuo kikuu cha Tumaini chaibuka kidedea katika michezo yote iliyochezwa katika viwanja vya chuoni hapo kwa kuwachapa wageni wao Mzumbe katika michezo yote iliyochezwa hapo ikijumuhisha mpira wa miguu,mpira wa pete,mpira wa nyavu pamoja na mpira wa kikapu.
 
      Katika mpira wa miguu Chuo kikuu cha Tumaini ilishinda magoli 3-0 katka vipindi tofauti na magoli ya mawili ya kwanza yalifungwa na mchezaji namba 4 SHIKIDE  na kipindi cha pili goli lilifungwa na na mchezaji namba 11 SELSUSE MPOTO. Hivyo mpaka dakika tisini za uwanjani Chuo cha Tumaini kilikuwa kinaongoza kwa magoli dhidi ya wapinzani wao Chuo kikuu cha Mzumbe.
       
      Kwa upande wa mpira wa pete Chuo cha Tumaini kiliweza ongeza kwa magoli 27 kwa 11 dhidi ya Chuo kikuu cha Mzumbe.Vilevile mpira wa wavu waliweza kuongoza tena kwa kuwafunga MZUMBE kwa seti 3 kwa 0(bila).Vilevile mpira wa kikapu Tumaini waliibuka tena kidedea.



                wachezaji wa chuo kikuu cha Tumaini wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi kuanza.




             
                    wachezaji wa Chuo kikuu cha Mzumbe 
     

No comments:

Post a Comment