Friday, May 25, 2012

Taswira:John Mnyika(CHADEMA)Mbunge Halali Jimbo La Ubungo


 Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA), John Mnyika akiwa amenyanyuliwa juu na wafuasi wa chama hicho baada ya kushinda kesi.
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. John Mnyika akiwa amebebwa juu juu na Wanachana wa Chama hicho pamoja na washabiki wake nje ya Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam leo mara baada ya kushinda kesi yake iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na Ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
 Mbunge wa ubungo John Mnyika katikati akiingia Mahakamani jana
 Mh. Mnyika alipokuwa akiwasili Mahakamani jana asubuhi.
  Mnyika akipongezwa na Baadhi ya jamaa zake waliofika Mahakamani hapo.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akipeana mkono na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
  Baada ya kutolewa kwa hukumu na Jaji Upendo Msuya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wapenzi na mashabiki wa Chadema walilipuka kwa furaha.
 Baadhi ya wafuasi wa CCM wakiwa Mahakamani.
Baadhi ya Waandishi wa Habari, wa pili kulia ni Happiness Katabazi kutoka Tanzania Daima
Baadhi ya wafuasi wa Chadema wakiwa nje ya jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania jana asubuhi katika kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Hawa Ng'umbi.
 Askari Polisi wakihakikisha usalama upo wa kutosha katika njia walizokuwa wakipita wapenzi wa Chadema kusherehekea ushindi wa Mbunge wao

No comments:

Post a Comment