Waziri
wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud
akielezea jambo kwa Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God
Zanzibar Dickson D,Kaganga wakwanza kulia kuhusiana na kuchomwa moto kwa
Kanisa hilo liliopo Kariakoo Mjini Zanzibar katikati ni Mkuu wa Jeshi
la Polisi I,G,P Saidi Mwemwa.
Mku
wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwema akitoa hotuba kwa Maaskofu na
baadhi ya waumini wa Kikristo katika kanisa la Tanzania Assemblies of
God Zanzibar lililochomwa moto,ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na
baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.kuliani kwake ni Mkuu wa Mkoa wa
Mjini Abdalla Mwinyi na kushoto yake ni Kamishna wa Jeshi la Polisi
Zanzibar Mussa Ali Mussa.
Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Abdalla Mwinyi Khamis akitoa
hotuba na kuonyesha Umoja na Mshikamano uliokuwepo kati ya Waislam na
Wakristo kwa Picha ambayo imebuniwa na Mchoraji wa kingereza na kuwataka
kuendelea na mshikamano wao ili kuzidi kuleta amani nchini.
Askofu
wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga
akielezea kwa Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mohd Aboud na Viongozi wengine mbalimbali kile kilichotokea
baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar
ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa na tokeo
hilo.
Askofu
wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga
akibubujikwa na Machozi kwa kuguswa na hotuba iliokuwa ikitolewa na
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud
baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar
ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa na tukio
hilo.
Mkuu
wa Dini ya Kiislam Afisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Noman Jongo
akitoa hotuba ya Dini inavyoeleza kuhusiana na kudumisha Amani na
Usalama katika nchi na kuondosha mifarakano na chuki na kuharibu
mali.Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar ambalo
limechomwa moto.
Askofu
wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga
akimuonesha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud
maeneo yalioathirika zaidi baada ya Kanisa hilo kuchomwa moto katika
Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na
baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.Picha na Yussuf Simai-Zanzibar