Monday, June 11, 2012

Buriani Mzee Bob Makani,Daima tutakukumbuka mpiganaji

Na Solomon Ole Lekui


ALIYEKUWA Muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mohamed Bob Makani amefariki dunia, maafisa wa Chadema wamethibitisha.

Makani amefariki Dunia jioni ya leo jijini Dar kwenye hospital ya Aghakhan, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amethibitisha hilo kwa njia ya simu kutoka Kanda ya kusini walikokuwa wakifanya mikutano yao ya hadhara.

Mbowe amesema Marehemu Makani alikuwa akiugua kwa muda mrefu na kupelekwa hospitali mbalimbali kwa matibabu ikiwemo nje ya nchi.
Amesema mwili wa Marehemu umehamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa hifadhi. Msiba upo nyumbani kwake Mbezi Beach jirani na Rainbow.

 Watu wakiaga mwili wa marehemu Bob Makani
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiwa na viongozi wakuu wa Chadema, Freeman Mbowe (mwenyekiti) na Dk Willbroad Slaa (Katibu) kuuga mwili wa marehemu Bob Makani, leo Karimjee.


Ukalale mahali pema mzee Bob Makani

No comments:

Post a Comment