Saturday, June 30, 2012

DOKTA ASHA-ROSE MIGIRO AWA MJUMBE WA MASUALA YA UKIMWI BARANI AFRIKA.


       Na Consolata Haule
         
      Aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa  Afrika dokta Asha-Rose Migiro         ameteuliwa    na katibu mkuu wa umoja wa mataifa   mheshimiwa Ban Ki Moon kuwa mjumbe wake maalum wa masuala ya Ukimwi barani afrika baada ya kumaliza mda wake.
    
       Alitangaza uteuzi huo katika hafla ya maaulum  aliyoondaa kwa ajili ya ya kumuuga Naibu Katibu Mkuu wake  ambaye amemaliza muda  wa uongozi  wake kwa muda wa miaka mitano na nusu katika nafasi ya  Unaibu Katibu  Mkuu.
  
        Hafla hiyo ilifanyika  katika wiwanja vya Umoja wa Mataifa na kuweza kuhudhuria na  wageni waalikwa wengi  mabalimbali na mashuhuru duniani wakiwemo mabalozi wan chi mbalimbali, wakuu wa mashirika  ya Umoja wa Mataifa. 
     
   Ametangaza rasmi kwamba amemteua dkt.  Asha- Rose Migiro kuwa  mjumbe wake maalum katika masuala ya ukimwi na ugonjwa wa Ukimwi Barani  Afrika. aliongeza kwa kusema  Ban Ki Moon. aliendelea kwa  kueleza kwamba ingawa Migiro alikuwa naibu katibu mkuu wake, lakini amekuwa mwalimu wake, na amejifunza mengi toka kwake na daima ataendelea kuuenzi mchango wake mkubwa aliofanya pindi alipokuwa kazini.

   “ Kama ni kuvaa viatu vyake, naweza kusema ningechekesha sana,  kwa ufupi siwezi kuvaa viatu vya Migiro, amekuwa msaada mkubwa sana kwangu, ameniwakilisha vema kila mahali nilipomtuma hata katika mazingira magumu na ya hatari,  kote ameniweza kuniwakalisha vema kiukweli. kama  mwalimu wangu, na kama profesa wangu anastahili alama ya juu sana” alisema  Ban Ki Moon na kushangiliwa.

   Alizidi kumuelezea  Migiro kama kiongozi si tu mwadilifu, lakini mwanadiplomasia  aliyebobea, aliyefanya kazi kubwa,ngumu na nzito kwa moyo mkunjufu, uhodari , umakini, na uadilifu wa hali ya juu sana.

    “ Siyo rahisi kuelezea yale aliyoyafanya nyuma ya pazia, namna gani alivyochapa kazi kwa nguvu, yapo mengi makubwa ambayo Migiro ameyafanya na  kuyakamilisha kwa uadilifu wa hali ya juu. Migiro ni mwanadiplomasia aliyebobea lakini ni mtu wa vitendo, vitendo ambavyo lazima utaona matunda yake” akabainisha Ban Ki Moon.

    Na kuongeza “  Migiro amefanya kazi na viongozi wagumu,  akiwemo aliyekuwa  Rais wa Libya Muammar  Quadaff aliyethubutu hata kumrushia katiba ya Umoja wa Mataifa, kiukweli ameweza kuzikuna nyonyo za watu wengi wakiwamo watu wanyonge na wenye matatizo mbalimbali duniani.Vilevile ameweza  kuondokana migogoro inayoendelea duniani. hivyo lakini Umoja wa  Mataifa hautasahau mchango wake.

      Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  alliweza kuitumia fursa hiyo  kwa kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini ya raisi wake Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumruhusu Migiro kwenda kuitumikia jumuia ya kimataifa.

   “ Ninapenda  kutoa shukrani zangu za pekee kwa  jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa kumtoa Migiro katika utumishi wake wa Umma kuja kunisaidia , kwa serikali ya Tanzania na  watanzania nasema asanteni sana” alisema Ban Ki Moon..

     Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu dkt. Asha-Rose Migiro amesema anaupokea kwa mikono miwili uteuzi wa kuwa mjumbe maalum wa Katibu Mkuu katika masuala ya Ukimwi barani Afrika.

      Alizidi kusema   masuala ya  ukimwi na ugonjwa wa ukimwi, ni eneo ambalo limo ndani ya moyo wake na kwamba anashukuru kuona kwamba Katibu Mkuu anamuamini anaweza kumsaidia. Aliaahidi  atalitekeleza  jukumu  hilo kwa heshima  kubwa aliyopewa na Katibu Mkuu.
       Pia alimshukuru Ban Ki Moon kwa kumuamini kwamba anaweza kumsaidia kama naibu Katibu Mkuu, na akamshukuru pia kwa ushirikiano mkubwa na uhusiano mkubwa uliojengeka kati yake na Ban Ki Moon lakini pia kati yake na wasaidizi wake.  Ushirikiano ambao alisema ulichangia utendaji mzuri wa kazi na kufanikisha dira na matarajio ya Katibu Mkuu.

      “Katibu Mkuu amenipa heshima ya kihistoria, heshima ya kuwa msadizi wake,  ni heshima kubwa kwangu na kwa yeyote atakayekuja kuandika historia yangu, kwa namna yoyote ile hawezi kukwepa  kumtaja  Ban Ki Moon, naomba nikushukuru sana kwa heshima hii kubwa uliyonipa” alisema Migiro.

      Katika hafla hiyo pia ilihudhuriwa  na familia ya Naibu Katibu Mkuu ikijumuisha  mume wake, Profesa  Cleophas Migiro,  mdogo wa  Naibu Katibu Mkuu, Bi. Amina  Mtengeti na mtoto wao wa  mwisho wa Migiro Chansa Jasmin.

    Naibu Katibu Migiro anakuwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo na mwanamke mwafrika wa kwanza. Lakini pia ni naibu katibu mkuu ambaye amehudumu katika wadhifa huo kwa miaka mitano na nusu.
Dokta Asha-Rose Migiro akizungumza na kutoa shukrani katika hafla hiyo.

         Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa anazungumza na wageni waalikwa hawapo pichani,kulia  ni Dkt. Migiro na katikati ni Mkurugenzi wa ofisi ya Naibu Katibu Mkuu, Bwana  Anyanga

No comments:

Post a Comment