Na Consolata haule
Coca-Cola Tanzania imetangaza kuanzisha tuzo kwa waandishi bora wa
michuano ya soka ya vijana ya Copa Coca-Cola kwa nia ya kuwazawadia
wanahabari wanaofanya kazi nzuri katika michezo,hivyo kuwa chachu ya mashindano ya Copa-Cola
yenye lengo la kujenga
msingi wa maendeleo ya soka nchini Tanzania.
Akizungumza na wandishi wa
habari jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa Coca Tanzania Salome Mabirizi
alisema kuwa Coca-cola inatambua mchango mkubwa uliofanywa na waadishi wa habari
kwa miaka mitano iliyopita katika kuwahamasisha kushiriki mashindano haya. Kuanzishwa kwa tuzo hizi ni njia moja wapo ya
kuwashukuru waandishi wa habari kwa kazi nzuri ya kutangaza Coca-Cola.
Alizitaja tuzo
hizo kuwa ni mwandishi bora wa magazeti, mwandishi bora wa luninga, mwanahabari
bora wa radio, mpiga picha bora (magazeti) na blogs bora, ambapo kila mshindi
ataweza kuzawadiwa thamani ya milioni 2 taslimu za kitanzania.
Mchakato wa kuwapata
washindi utafanywa kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa Habari za Michezo
Tanzania (TASWA) na Coca-Cola na tayari zoezi hilo limeshaanza tangu Jumapili
juni 24 wakati fainali za Copa Coca-Cola Taifa zilipozinduliwa rasmi jijini Dar
es Salaam na Fainali hizo zimepangwa kumalizika Julai 15.
Katibu Mkuu Msaidizi wa
TASWA, George John aliwaambia waandishi wa habari kuwa kamati ya tuzo za Copa
Coca-Cola itafanya kazi kwa kuzingatia vigezo ili kuweza kumpata mshindi anayestahili
katika kila kundi lililotaja hapo juu.Pia amevitaja baadhi ya
vigezo hivyo kuwa ni pamoja na stori au makala zinazohamasisha na kuwatia moyo
vijana kuweza kuonyesha na kuendeleza vipaji vyao.
Johan ameipongeza kampuni
ya Coca-Cola kwa kushirikiana na Shirika la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
kuendesha mashindano hyo kwa nchi nzima kwa lengo la kuibua vipaji vya wanasoka
chipukizi nchini Tanzania.
Kiukweli Copa Caca_Cola imesaidia
kubadili sura ya mpira wa miguu nchini Tanzania kwa kuwa chanzo cha kutegemewana wachezaji wenye vipaji wa kila timu za ligi kuu na timu za Taifa.
NI mashindano pekee nchini ambayo huchezwa nchi
nzima kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa yakishirikisha maelefu ya vijana kila
mwaka ili kuwaendeleza vijana
zaidi.
Coca-Cola imekuwa ikipeleka
wachezaji bora wa Copa Coca-Cola kwenye kambi za kimataifa za mafunzo ya soka
nchi za nje. Mnamo Mwaka 2007 na 2008
wachezaji bora wa Copa Coca-Cola walikwenda nchini Brazil na kuanzia 2008 hadi
mwaka jana walipelekwa Afrika Kusini.
Coca-Cola ni kampuni yenye
historia ndefu ya kusaidia michezo ilianza kudhamini michezo ya olimpiki tangu
1928 na mpira wa miguu tangu 1930.
Kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikidhamini Shirikisho la mpira wa miguu
duniani (FIFA) tangu 1974 na kuwa mdhamini rasmi wa FIFA tangu 1978 hadi sasa.
Mkurugenzi mahusiano wa Coca Cola Kwanza( wa katikati )Bw. Evans Mlelwa
akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za Coca Cola juu ya Tuzo kwa waandishi wa habari COPA COCA
COLA,wa kwanza kulia ni Katibu msaidizi wa Taswa Bw. George John,kwa upande wa kushoto ni Meneja Masoko wa Coca Cola Tanzania Bi.Salome Mabirizi.
No comments:
Post a Comment